Kuna wanaume wanaishi kwenye ndoa ngumu nyie

Kuna wanaume wanaishi kwenye ndoa ngumu nyie

.......kamdhalilisha pakubwa sana na jinsi clip inavyotembea chap, ndugu wa Jamaa sijui wanajisikiaje huko.......wapo wengi wanaodharau waume zao lakini huwa hawaoneshi nje kiasi hicho, hata hapo wapo, kaharibu sana......
Yaaani pengine ni mihemko
 
Lile pambio lenu la KATAA NDOA limesambaratishwa na massively atomic bomb, hadi sasa hivi timu KUBALI NDOA 3-0, nimekaa pale [emoji144][emoji4]

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Kama huyu mwanamke wa Mchechu bado utakubali kuna ndoa hapo. Haujapitia nyuzi za karibuni kuhusu ndoa nini? Watu wanalia humu ndoa hazieleweki, fuatilia ujionee
 
Kuna tofauti kati ya kuaga na kutoa taarifa. Kuaga kuna nafasi ya kuambiwa usiende..!! Kutoa taarifa ni amri kwamba liwalo na liwe lazima uende..!!

NB:
KUNA TOFAUTI KATI YA MKE MWEMA NA MWANAMKE MPAMBANAJI....!!! Huyu wa kupambana, huwa anapambana hadi na mumewe. Mke mwema huwa mtiifu wakati wote..!!

Sasa ukute mwanamke kama huyo (wa kupambana na mumewe) awe ana madaraka, ana hela na ana shule kubwa..!! Lazima patachimbika..!!

Na wanawake dezaini hii, ndo wanafanya jaami ione kuwa ukmpa mwanamke uwezo, lazima aote kiburi cha kutaka kupambana na yeyote yule, hata mahala panapohitaji busara ndogo tu.
Mtu mzima haagi anatoa taarifa. Ndio maana alipotoa taarifa mumewe hakuwa na shida. Shida iko kwenu wenye mitizamo potofu.

Hivi sio nyie kila siku mnaropoka kutaka wanawake financial independent? Au huwa ni uchoyo unawasumbua kumbe deep within hamko tayari kwa wanawake hao!!!
 
Shemela Evelyn Salt, Bantu Lady, Mideko, lovely love, Kapeace, binti kiziwi, Dejane, Kalpana, Lanlady, Lovelovie, Numbisa, Mamndenyi etc embu elezeni kama huyu mama yupo sawa au la..!!
Katika zama hizi za mwanamke kuwa na uchumi, kuzidi mume..
Hapo kinachotakiwa ni upendo tu, unajua ukiwa na upendo kwa mwenza wako, hata umzidi kipato still utamuheshimu.

Sasa huyu hata huo upendo hana, anachoangalia yeye ana uchumi wake vizuri so anaweza kufanya lolote, na mume asiseme lolote.
Kweli wanawake tumewezeshwa, tumeweza. Kama unataka kuwa na mwenza ama ndoa yenye furaha, tanguliza upendo kwake.

Muishi kwanza kama marafiki, wapenzi na mume na mke. Mama hapo kakosea na siwezi fata mafundisho yake. Wee my man nampenda, niache kumpa taarifa mapema, hata anisaidie kunichagulia nguo kimahaba, aniambie jinsi ilivyonikaa na nilivyopendeza. Kuna watu hawajuhi mahaba bana kaa huyo bi hambiliki...
 
Huyu dada Mercy Luhanga. Mke wa Nehemia Mchechu. Ngonja nikamnyakie Mchechu nimpe heshima zote na mapenzi kama yote. Hahahhaha.Mbona Mercy atatia akili.Jamani ninatania tu,nimeokoka siwezi iba mme wa mtu.
Victoire nami nimeokoka, tukutane hapa kwa Massawe tupongezane furaha ya wokovu tulionao.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom