babukijana
JF-Expert Member
- Jul 21, 2009
- 14,478
- 18,341
Acha tu kuna siku nimekatiza mahali tunaenda mpirani naona gari hii hapa.Mzee alikuwa baharia huyo anazuga na chumvi kumbe anaenda kula mzigo 🤣🤣🤣!!! Kijana unachekelea paja za kuku na kidali mama yako anaenda kuinjoy ndani 😀 wazee mabaharia wanapendwa sana. Sema sahizi hamna matoleo kama yale tumebakia mabaharia wachache sana.
Nikaona hapa mi nazama ndani namkuta.
Dingi vp?
Aah mi nazuga tu hapa,
We umefata nini huku?
Naenda mpirani
Aah mwanangu twende hapo nikurekebishie.
Kanipa mazaga kibao.
Nikamwambia mkeo anakusubiri kule.
Karekebishe.
Hapo najua menu ntaikuta😅😅😅
Naenda jembe langu ila usimwambie umenikuta huku.
Poa.
Miaka ya 80 hapo hamna simu upige.
Ile siri mpk leo sijaisema kwa maza