Bado tupo wapenzi wa kusikiliza redio,
Mfano, nusu ya Mechi za kombe la Dunia la 2006 Germany, nimezisikiliza kupitia redio na Charles hirari Mtangazaji.
Hivi Sasa Huwa nipo na radio Maisha Kutoka Kenya, watangazaji Steve Mkangai(baba Nora man of tactics , Nyota wa kumemetuka uwanjani,na Hassan mwana wa Ali (Japo kahama redio)
Bila kusahau vituko vya Amope vya Hassan mwana wa Ali.
Mfano wa kituko Cha Amope,
"Amope amekaa Miaka sita analalama hana kazi, ghafla bin vu Amope anabadilika viatu bei ghali, nguo bei ghali, simu bei ghali, nyumba bei, usafiri bei ghali, wenzake wanamuuliza mwenzetu unafanya kazi gani,
Amope anasema njooni niwaonyeshe, wanapokaribia kwake anafungua simu yake anawaonyesha mtandaoo wa betting, anasema Hii ndioo ofisi yanguu, hahaha "
Watu tumeanza kusikiliza redio, Idhaa ya kiswahili, Dw, Voa, R na nk, tukiwa vidudu,
Mpaka tumekuwa kama wa raibu.
Siku haiwezi kutamatika bila kusikiliza idhaa ya kiswahili hata Moja na kupata mbili tatu taarifaa na changanuzi za ulimwengu na matukio yake.