Kuna watu wana miaka 30 na bado wapo nyumbani kwa wazazi, nimelia sana

P h a r a o h

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2024
Posts
785
Reaction score
1,413
Miaka 30 ni mingi sana kukaa hapa duniani sio tu kukaa nyumbani, inabidi uwe umesha leta impact.

Kuna watu kabla ya hiyo miaka walishafanya makubwa sana hadi sasa bado wanakumbukwa kwenye historia ya Dunia.

Unamjua Alexander the Great, aliyoyafanya yote hadi kutawala almost Dunia nzima Aliya fanya kabla ya kufikia miaka 30 na alikufa akiwa 30'S, ila hadi saivi anakumbukwa na hawezi kusahaulika kwenye historia ya Dunia ingawa aliishi B.C huko.

Huo ni mfano mmoja tu ila ukiwa na miaka 30 inabidi uwe umeshafanya mambo makubwa tuu, hata kufa tayari, kama kina kanumba etc.

Fanya kitu leta impact amsha, kwani wewe ulikuja Duniani ku enjoy tuu?

Muda ni mchache sana, kama ulitaka kukaa milele si ungekua mlima, au hata uwe kobe uishi miaka 200+! Binadamu aliumbwa akapewa akili ili aje kuleta impact kwenye Dunia au wewe utashabikia tu Simba na Yanga, "Stop existing start living."

Kwa wataoniuliza mimi nimefanyaje na nina miaka ngapi mimi nina miaka 12!
 
Wewe unasema kwenu USWAZI, and you must be living in Uswazi

Kuna wazazi wana nyumba kama apartments............kila mmoja na kweke ila mnakutana katika mambo ambayo mmekubaliana kuwa pamoja eg mnaweza kukubaliana milo yote ni ya shirika...kuna employed people for that kama wanavyoishi mapadre wa kikatoliki....nimeona familia zinazoishi hivyo.
 



Moja ya mambo huwa yamewashinda kuyaelewa watu ni kufananisha Umri na mafanikio.

Miaka 30 unaweza ukawa hauna kitu chochote unachomiliki ,ikiwemo ,kazi, elimu, familia , n.k

Ila miaka 31 ukajikuta Una kila kitu.

Hapa duniani huwa hakuna umri wa kufanya jambo Fulani Ila huwa kuna wakati na majira ya kufanya jambo Fulani.

Jambo la muhimu ambalo kijana anabidi kuwa nalo ni kuwa sober 24/7

Umri huwa haumfanyi MTU afanikiwe wala asifanikiwe

Unaweza msoma hata founder wa KFC katoboa Ana miaka 65+yrs
 
miongoni mwa tabia na utambulisho wao wa mwanzo Kabisa ni mihemko, ghadhabu na matusi ukimchalenge kidogo tu juu ya maisha 🐒

ni wakali mno hasa wakiona wa age ya 25 katoboa 🐒
 
Dump🚮
 
Tena siku hizi ndo wengi sana. Vijana hadi miaka 40 wasengea kwa wazazi. Mimi nilitoka kwa wazazi baada tu ya kuimaliza form six, nikatafuta tempo ya kufundisha na kupanga geto na hapo hapo nikaanza kuwasaidia wawazi wangu kulipia baadjhi ya mahitaji ya shule wadogo zangu. Ndivyo safari yangu ilivyoanza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…