Kuna watu wanauawa bila Hatia kwa tuhuma za wizi, watanzania tuache kukurupuka

Nimeona acha nichangie maana imenigusa mno!
Haya maswala yanatokea sana na wengi wamepoteza maisha burebure tu.
Jambo kama hili sio la kufumbia macho sababu wewe unaekurupuka iko siku pia ndugu yako atafanyiwa hivyo!
Ni mfano mbaya hata ukipita sehemu ukakuta mtu amevamiwa na vibaka au majambazi ila kwakuwa mtu huyo hakuhusu au humjui unapita bila kutoa msaada wowote nakuhakikishia ipo siku utapita wewe utafanyiwa hivyo au ndugu yako au rafiki.tuache kupuuzia mambo ambayo baadae yatarudi na kutuwinda wenyewe
 
Najivunia lugha yangu ya kiswahili hivyo sina budi kuithamini na kuipenda nashukuru kwa kunirekebisha!!! Amani iwe nanyi daima
 
Umenena vema sana mkuj
 
Mkuu hii "Elimu" jaribu kuisambaza kadiri uwezavyo ili iwafikie watu wengi zaidi,nasi tutakusaidia kuisambaza ili isomwe na watu wengi zaidi ikiwa utaturuhusu kuisambaza.
 
Mkuu hii "Elimu" jaribu kuisambaza kadiri uwezavyo ili iwafikie watu wengi zaidi,nasi tutakusaidia kuisambaza ili isomwe na watu wengi zaidi ikiwa utaturuhusu kuisambaza.

CleverKing umekuwa mchangiaji muhimu na umetoa ushauri mwingi mzuri na wenye mafunzo
Nafikiri hapa pia ni mahali sahihi pamoja na majukwaa mengi zaidi,
Nitajaribu kutumia shuhuda za kusikitisha walizotoa wachangiaji ili kuweka mtiririko wa matukio unaoleta hisia zinazogusa watu.
Nakaribisha maoni na ushauri toka kwenu kwani KAZI HII INATUHUSU SOTE mkuu
 
Mtukufu wao kawambia wamnyanganye silaha haraka haraka...yaani hukumu bila hata mahakamani hajafikishwa.
Hakika viongozi huchangia sehemu kubwa ya uvunjaji wa sheria na hakuna mwanadamu aliyepewa haki ya kutoa uhai wa mwingine zaidi ya mwendo kasi decesions tu.
Vizuri ndugu kwa kuokoa uhai wa mtu huyo.
 
Cleverking hebu pitia shuhuda za hawa wachache zinazoashiria ukubwa wa tatizo hili la kufanya maamuzi pasipo kujiridhisha kama ni ya kweli.
Hayo hayo ya kukurupuka jamaa mmoja Mbeya aliuwawa kwa kuhisiwa anaiba mbuzi kumbe alimkuta mbuzi amejikaba shingo kamba imemnyoga anataka kufa akaamua kumnasua. Watu walipomkuta anamnasua mbuzi wakaita mwizi kisha?.....kipigo hadi kufa.


Kuna uzi niliuona umu jana kijana kapigwa risasi tatu mguuni kisa kama baada ya tukio wanasema sio mwizi mpaka sasa cjafahamu kijana wa watu anaendeleaje inauma sana kwa kweli


Daaa nimemkumbuka class mate wangu Edwin Macha aliuawa kwa kusingiziwa mwizi! Rest in peace bro


Mkuu hii "Elimu" jaribu kuisambaza kadiri uwezavyo ili iwafikie watu wengi zaidi,nasi tutakusaidia kuisambaza ili isomwe na watu wengi zaidi ikiwa utaturuhusu kuisambaza.
 
Watanzania wengi wetu ni wafuata mkumbo ukiona furani anacheka na wewe unaaza kusaidia kucheka bila kujali ni nini kinachomchekesha yule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…