Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Sabato Njema!
Jana baada ya kuandika uzi fulani ambao niliomba Mtu fulani kutolewa Jela septemba kabla ya tarehe 7. Mtu mmoja aliyejitambulisha kwa jina gumu sana alinitokea. Yule mtu akaniambia kuwa sipaswi kuandika tena habari hizo wala sipaswi kuwabembeleza watu hao. Kwani wameamua kushindwa hivyo hawatanisikiliza.
Nikamuuliza nini kitatokea, akaniambia Watashushwa chini, chini kabisa.
Nikauliza chini, chini kabisa ndio wapi na nini? Akanijibu, Chini, Chini kabisa kwenye giza mahali ambapo wenye macho na wasio na macho huwa kitu kimoja. Wenye masikio na wasio na masikio huwa kitu kimoja.
Nikauliza swali la mwisho, itakuwa lini na nitajuaje?
Akanijibu sitajua pekeangu kwani litakuwa tukio la wazi kila mtu ataliona na atashangaa. Utakuwa ufagizi wa ajabu wenye ghadhabu isiyozuilika lakini mmoja wao hatashuka chini, yeye ataugua ugonjwa wa kulala muda mrefu kitandani. Na nafasi yake itachukuliwa akiwa anajitambua akiwa kitandani.
Nikauliza, je hiko ndio kile kisasi cha yule wa Arusha?
Akasema hapana, Yule wa Arusha ataleta Ufagizi wa Pili kabla naye hajafagiliwa.
Basi Nikaamka natazama ilikuwa saa 11 alfajiri. Wala sikutaka kuiwaza wala kuitafakari. Nikaenda zangu Kanisani kuabudu na kumwomba Mungu.
Mungu wa mbinguni awabariki Sana.
Na hili sio Fasihi!
Nataka nione ni Makande au mtu yule mwenye jina gumu ni mkweli au anatania.
TaikonMaster
Kwa Sasa Dar es salaam