Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
KUNIZUNGUSHA SANA SIO KAMA NDIO NITAKUONA WEWE SIO MALAYA AU SIO RAHISI.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli
Moja ya mambo ambayo yananifanya nimshushe mwanamke nyota zake hasa za kiutambuzi na kumwona ni wale wanawake wa standard za kawaida ni kuwa na mtazamo usemao kuwa kumzungusha mwanaume au kutokumkubalia haraka mwanaume ni kulinda brand na ataniona ninamaadili au ni mwanamke asiye Malaya
Watibeli tuna- prefer mwanamke ambaye atakubali siku hiyohiyo hata kama ni malaya kuliko asiye Malaya ambaye atakubali baada ya mwezi mmoja... Kwa sababu ya kijinga kubwa akikubali siku moja ati nitamwona Malaya.
Ni mwanaume mjinga atatumia kigezo cha siku za kukubaliwa kama kipimo cha tabia ya mwanaume. Kwamba kuzungushwa sana kunaashiria msimamo wa Mwanamke.
Mwanamke mwenye msimamo hana huo muda wa kukuzungusha. Kama hakutaki ni hakutaki. Kukuzungusha ndio umalaya wenyewe.
Kama anakupenda ukimtongoza atakubali siku hiyohiyo.
Mwanamke au mwanaume anayeangalia wengine watamwonaje huyo hafai kwenye mahusiano yenye afya. Anaigiza, ataigiza na kutaka kukupa kile watu wanachotaka huku tabia zake akizificha.
Mwanamke mwenye akili timamu majibu yake ni;
1. Kama hakujui ndio mmekutana paaap! Akakuelewa, ukamtongoza atakubali mpeane mawasiliano na ukitaka jibu atakuambia ukweli kuwa anakuelewa vizuri sana na wewe ni type yake ingawaje bado hakuamini.
Kama hajakuelewa, atakuchana mapema kuwa sikutaki na sikupendi. Na mwanaume mwenye akili ataelewa na kufanya mambo mengine.
2. Kama mnafahamiana kwa muda mrefu labda ni workmates, au classmates au mnaishi mtaa mmoja, au mnasali pamoja. Ukimtongoza, atakujibu siku hiyohiyo kubwa nakutaka, nakupenda na pia nilikuwa na kuhitaji. Simple.
Kama hakutaki atasema.
Kisha mtapanga utaratibu wa mahusiano yenu yaendeje. Na hiyo ni siku hiyohiyo.
Lakini ukishaona kona kona, sijui na kufikiria, sijui subiri nitakujibu, sijui bla blah.
Sijui nikuchunguze. Huo ni utapeli.
Huo ndio umalaya wenyewe sasa.
Ni sawa na Mwanamke upo kwenye mahusiano ya uchumba na mwanaume unamwambie vipi kuhusu kuishi pamoja iwe kwa ndoa au taratibu zingine aanze kupiga piga chenga. Unapiga chenga nini.
Hiyo ni red alert. Ni ishara kubwa ya kupigwa na kitu kizito.
Taikon ninakufuata labda Kalpana
Nakutongoza, najua una standard zako, unatype zako, nakutongoza,
Kama hutaki sema hutaki, sema unamtu wako. Sema mimi sio chaguo lako.
Sio ulete mambo ya kitoto.
Yaani unataka alafu unajifanya hautaki. Kwamba?
Iko hivi, mwanamke uliyemfuata leo akakukubalia siku hiyohiyo nina kuhakikishia una asilimia 90 ya kudumu naye na kuwa na furaha kwa miaka mingi tofauti na yule atakayekuzungusha miezi kadhaa.
Mwanamke anayekukubalia siku hiyohiyo ni mwaminifu zaidi kuliko atakayekuzungusha alafu baadaye ndio akubali. Hapo hakuna kitu hapo.
Kumbuka, kukubaliwa kimahusiano haimaanishi kumvua chupi siku hiyohiyo.
Kuvuana chupi ni jambo jingine.
Mwanaume anapokuja kukutongoza kama ni type yako na unampenda mkubalie.
Kisha mengine ndio yafuate.
Kama anakutongoza alafu siku hiyohiyo anataka akuvue chupi basi huyo atakuwa sio tuu amekudharau bali amekuona wewe ni kahaba.
Lakini ni kakuomba uwe mchumbaake/mpenzi wake na unampenda, unamkatalia kwa kigezo kipi alafu baadaye unamkubalia kwa kigezo kipi kama sio unafiki. Au utoto? Kutojiamini?
Wewe kama ni Malaya ni Malaya tuu. Hata umzungushe mtu miaka buku. Kumzungusha mtu hakukufanyi usiwe Malaya.
Umalaya unaanzia kwenye mtazamo wako kama mwanamke. Unavyojichukulia na vile unavyotaka watu wakuchukulie.
Kisha ndio matendo yako.
Acha nipumzike
Robert Heriel
TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam