KUMBUKUMBU LA SHERIA. 22 : 13-21
"Mtu akitwaa mke, akamwingilia na kumchukia, kisha akamshtaki mambo ya aibu kumzushia jina baya, akasema , Nimemtwamwanamke huyu, nami nilipomkaribia sikuona kwake alama ya ubikra;
Ndipo babaye na yule kijana na mamaye watakapotwaa alama za yule kijana za ubikira, wawatolee wazee wa mji langoni
Na baba yake yule kijana awaambie wazee, mwanamme huyu nilimpa binti yangu awe mkewe, naye mchukia;
Angalieni amemwekea mambo ya ajabu asema, sikuona kwa binti yako alama ya ubikira, nazo hizi ndizo alama za binti yangu za ubikira, na wayakunjue yale mavazi mbele ya wazee wa mji
Basi wazee wa mji ule na wamtwae yuke mtu mume na kumrudi.
Wamtoze shekeli mia za fedha wampe babaye yule kijana, kwakuwa amemzulia jina baya mwanamwali wa israel; naye awe mkewe, huna ruhusa ya kumwacha kwa siku zake zote.
Lakini ikiwa ni kweli neno hili la kutoonekana kwake yule kijana alama za ubikira
Na wamtoe nje yule kijana mlangoni pa nyumba ya baba yake, na waume wa mji wake wampige kwa mawe hata afe, kwa vile alivyofanya upumbavu katika israel, kwa kufanya ukahaba katika nyumba ya baba yake, ndivyo utakavyoondoa uovu katika ti yako.