Kuoa ni lazima?

Kuoa ni lazima?

mtume paul alisema si lazima kuoa ila kama una moyo wa kuishi na hawa viumbe oa nabii yesu hakuwa na manzi alielewa mohamadii alikuwa nao kibao ili kuepisha stres kapiga wanne.ila uzuri wa jack ulishawishi nvute ndani
 
Tukiweka masikhara pembeni, upweke unaumiza halafu unaua, itafika muda utawish tu uwe na partner wako ndani, leo mmecheka, kesho mmetibuana, ili mradi tu siku zinaenda,
Imagine upo kwenye mjumba mkuuubwa upo peke yako tu, kuna muda wa kula na muda wa kulala hapa wengi huwaza vitu vingi sana,

Ps: Ndoa sio lazima lakini kua na Partner wako (awe Me au Ke, wewe tu na chaguzi zako) ni muhimu kwa afya ya akili na mwili wako.
 
Kuoa sio lazima, lakini katika Uislam ni tendo la Sunna lililotiliwa nguvu...
بسم الله الرحمن الرحيم.
وَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تُقْسِطُواْ فِى ٱلْيَتَٰمَىٰ فَٱنكِحُواْ مَا طَابَ لَكُم مِّنَ ٱلنِّسَآءِ مَثْنَىٰ وَثُلَٰثَ وَرُبَٰعَ ۖ فَإِنْ خِفْتُمْ أَلَّا تَعْدِلُواْ فَوَٰحِدَةً.
Ikiwa mna khofu ya kutowafanyia wema mayatima basi oweni miongoni mwa mnaowapenda katika wanawake wawili na watatu na wanne, ikiwa ikiwa mna hofu ya kutowafanyia uadilifu basi oweni mmoja.

القاعدة
Katika Uislam mtoto wa nje ya ndoa harithi.

Urithi umeingiaje hapo, so ikiwa hujaoa ila unazo mali na watoto umezaa... inakuwaje hii!!
 
Shida gani mfano ambayo unaweza kuipata ndugu wa damu wakakukimbia lakini mke akawa na wewe?
Assume kwa mfano umepata kiharusi,ndugu zako wataweza kukuogesha,kukusafisha,kukubeba usiku wa manane kukupeleka chooni?
 
Sio lazima. Unaweza kuolewa pia [emoji3][emoji87][emoji2088][emoji13]
 
Urithi umeingiaje hapo, so ikiwa hujaoa ila unazo mali na watoto umezaa... inakuwaje hii!!
Hiyo ni kwa mujibu wa Uislam.
Ukiamua kufuata sheria za Mungu, mali watarithi ndugu zako.
Ukiamua kufuata unavyotaka mwenyewe pia fuata, mengine utakwenda kujua ukifika kwa muumba wako.
 
Swali linalotaka jibu sahihi.

Kama Mwanaume anapata kila anachotakiwa kukipata kwenye ndoa kwa njia mbadala, kuna haja ya Kuoa?

Sex atapata nje
Mtoto atamzalisha mtu
Kufua kuna Laundry
Out kuna Hunters
Kula hotelini,

Uzuri hapati stress
So lazima,
Kwa sababu huna adhabu ya kutooa Wala hukumu utakayohukumiwa chini duniani Wala juu mbinguni.
Mtume Paulo, kwenye waraka wake wa kwanza kwa wakorintho, nadhani sura ya 19,au 20 au 21 , amesisitiza pia kwamba jambo hili Ni maamuzi ya mtu binafsi.
Hata hivo , pamoja na sababu mbalimbali za kuoa kuwa na fumbuzi mbadala, Bado ndoa Ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa jamii, maana ndipo penye uhakika wa malezi Bora ya watoto.
Vinginevyo Ni ongezeko la watoto wanaolelewa na mzazi upande mmoja, ambalo ndio kwa kawaida hupelekea ongezeko la watoto wa mtaani..
 
Ndoa ni makubaliano kati yako na rafiki yako au mpenzi wako. Mfano mzuri ni kwa Adam na Hawa sidhani kama walienda kanisani au msikitini kufunga ndoa ila mungu tu kuwawakutanisha pamoja ni tayari walishakua wamekubaliana kuishi mpaka kufa pamoja
Hii tafsiri unaipata wapi ndugu yangu..!!
Hujui kuwa ndoa ipo kisheria?
Kwa hiyo Sheria ya ndoa inasema hivo???
Adamu na Hawa, ile Ni ndoa kwa mazingira yao,.na sasa tuna ndoa katika mazingira yetu ya sasa..
 
Watoto wazinaa waliozaliwa na wazazi wazinzi lazima watasema kuoa sio lazima
Naam..!!!
Tupe reference ya kisheria au kiimani inayoonesha kuwa kuoa Ni lazima , pamoja na adhabu au hukumu inayomkabili atakaebainika kutokufunga ndoa..
 
So lazima,
Kwa sababu huna adhabu ya kutooa Wala hukumu utakayohukumiwa chini duniani Wala juu mbinguni.
Mtume Paulo, kwenye waraka wake wa kwanza kwa wakorintho, nadhani sura ya 19,au 20 au 21 , amesisitiza pia kwamba jambo hili Ni maamuzi ya mtu binafsi.
Hata hivo , pamoja na sababu mbalimbali za kuoa kuwa na fumbuzi mbadala, Bado ndoa Ni muhimu kwa ajili ya ustawi wa jamii, maana ndipo penye uhakika wa malezi Bora ya watoto.
Vinginevyo Ni ongezeko la watoto wanaolelewa na mzazi upande mmoja, ambalo ndio kwa kawaida hupelekea ongezeko la watoto wa mtaani..
1 Wakorintho 7 : 9
"Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa."

1 Wakorintho 7 :10
"Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe;"
 
Back
Top Bottom