Pengine kijana wangu ila tatizo ni kuwa sitapenda kumchagulia mke maana mama yao ni chaguo langu na si la wazazi. Tuombe Mungu huenda mkakutana na mwishowe tukaja kufahamiana kumbe wewe ni Shishi wa JF.
Hapa poa we tulia tu tutaletana nyumbani lol.
Kama familia ina uwezo isione gharama kuhudumia mke na watoto wa kike. Vinginevyo hasa kwa mabinti zetu kama hutafanya hivyo atataka naye apendeze at the expense of nothing else but her body. Take it from me. Hata mabinti wakifikia 12 years anza kumhimiza mama yao wawe wanampa bajeti ya mahitaji yao. It is extremely important, na utamfanya asiwe na tamaa. Of course, hapa ni lazima uwe makini kukaa naye kupitia hiyo list kuona kweli it is ok. From the beginning unamfundisha ku-list yale mahitaji muhimu na awe mwaminifu na iwe mazoea. Kama mzazi utatumika pia kumlea binti kuwa mke mwaminifu si kama yule wa rafiki yangu Fidel80 sijui kimada au girlfriend anataka 70,000 za hair retouch. Nimechoka mbavu. Kama ni kwa ajili ya body cleaning saloon hiyo ni nyingi na unaweza kufanya pedicure, manicure, massage, facial, na mambo kibao wanamama wanafahamu watatutajia.