Sasa Shishi mimi huyu basi tena amenichuna vya kutosha naachana nae kabisa. Amenitumia sms oooh dear naomba ijumaa unisaidie laki moja kuna nguo nimeona Mr.Price,nimemjibu nimefulia.
Hehehe mtagombana na MJ1 shauri yako mi simo.
Huyu weekend hii simpi hata buku.
mh kumbe unanijali namna hii..... aksante
mh kumbe unanijali namna hii..... aksante
Yeah lazima nikupe kupaumbele kuna watu wananyemelea nafasi yako mama.
........... Ndo nawaona ila mh unahonga dau kubwa sana bana... unakumbuka ule wimbo
.... aisee mume wangu mie, anatoa pesa nyingi x 2
kuliko ile mahari aliyotoaaaa.........
teh teh teh Kwani Uchafu ni nini?Jamani tusiuane humu ndani,suala la usafi linategemea mambo mengi yakiwepo mazingira,utamaduni,kipato,malezi,imani,utashi wa mtu binafsi,hulka na mengine kama hayo. Ku generalize kwamba 'wanawake ni wachafu' au 'wanaume ni wachafu' tunakuwa hatutendeani haki.Wadau si mnajua kwa makabila mengine kujipaka udongo ndio usafi au kujipaka mafuta ya ng'ombe mazito yale ndo usafi.Linaloweza kuonekana kwako ni uchafu si ajabu kwa mwenzio ndo manjonjo. Tustahimiliane wadau!
Wenye mwelekeo kama Maane utawajua tu tangia uchumba.Ukiona mwanaume hana interest kujua unaji maintain vipi hata kama hakuwezeshi kifedha, ujue huyo ni bomu.Ukiona mwanaume kila mara anashangaa inakuwa vipi kila mara unataka kwenda salon au kwa beautician wako hata kama hatoi pesa mfukoni mwake..ujue mbele ya safari kuna shida.Ogopa mwanaume anayekushangaa kwanini unatumia pesa kwa ajili ya usafi wako binafsi, wake na familia - ati haoni kwanini ununue sabuni na shower gels, shampoo, bathroom cleaning agents etc akidai ati nunua Ommo au mbuni ni multi purpose utajuuuuuta kuolewa nae baadae!
You single ladies out there, msiseme hamkuambiwa!
Nimejaribu kuufuata moyo wangu lakini inaonekana namkwaza mwenzangu.Mazingira niliyokulia bwana kuingia pamoja bafuni na mke wangu inaniwia ugumu kweli..najitahidi kujifunza kukubali kama nilivyoweza kujifunza calculas na algebra na chemia na kila kitu.Wewe binafsi unaonaje? Fuata moyo wako wala usijali wengine wanafanya nini.
mmm Maane mbona watutia wivu we nawe...hivi mdogo wako yupo???? ahahahhaha. but am very impressed kwa kweli ni wachache watafanya hayo yote.. kazi kukwambia tangu tuoanane u no longer have a waist line duhhh mijiume mingine bwana!!! ukisema wataka cleanser waambiwa ya pesa nyingi halafu akitoka nje wanatawatamani wale wenye nyuso kama za watoto...hapo patawezekana kweli???
Pengine kijana wangu ila tatizo ni kuwa sitapenda kumchagulia mke maana mama yao ni chaguo langu na si la wazazi. Tuombe Mungu huenda mkakutana na mwishowe tukaja kufahamiana kumbe wewe ni Shishi wa JF.
Hapa poa we tulia tu tutaletana nyumbani lol.
Kama familia ina uwezo isione gharama kuhudumia mke na watoto wa kike. Vinginevyo hasa kwa mabinti zetu kama hutafanya hivyo atataka naye apendeze at the expense of nothing else but her body. Take it from me. Hata mabinti wakifikia 12 years anza kumhimiza mama yao wawe wanampa bajeti ya mahitaji yao. It is extremely important, na utamfanya asiwe na tamaa. Of course, hapa ni lazima uwe makini kukaa naye kupitia hiyo list kuona kweli it is ok. From the beginning unamfundisha ku-list yale mahitaji muhimu na awe mwaminifu na iwe mazoea. Kama mzazi utatumika pia kumlea binti kuwa mke mwaminifu si kama yule wa rafiki yangu Fidel80 sijui kimada au girlfriend anataka 70,000 za hair retouch. Nimechoka mbavu. Kama ni kwa ajili ya body cleaning saloon hiyo ni nyingi na unaweza kufanya pedicure, manicure, massage, facial, na mambo kibao wanamama wanafahamu watatutajia.
mke mwaminifu si kama yule wa rafiki yangu Fidel80 sijui kimada au girlfriend anataka 70,000 za hair retouch. Nimechoka mbavu.
kwa kweli hiki ni kitu cha muhimu, usipomtimizia bintiyo haya mahitaji ndio anakwenda chuoni kukutana na kina Fidel na YoYo.....mfano tu jamani msiniue mwenzenu! kumbe malezi pia muhimu sana!! ahsante sana kwa hiyo shule hapo!
Hehehehe akija chuoni akikuatana na sie si tunasaidiana kulea kwani kuna tatizo? Si kama huyo naye mpa 70,000/= kwa wiki kwa kutengeneza nywele tu.
Ni ubwege tu, ukiona hivyo ujue hamna plan ya maana ya kufanya au hamko bussy
Nina home work kubwa sana kupata mke/mchumba mwaminifu yaani ni kazi kweli kweli Bro. huyu ananikamua sana tena hiyo sabini nayo toa bado analalamika akitoka saloon nakuta uso na nywele za kawaida tu sijui ni usafi au nini sielewi ananidanga tu anatumia vipodozi vya Japan ni ghali sana kuliko vya US au South Africa.
hahahahhahahaha WoS umenimaliza kabisaaaaa Mungu wangu kweliii mbona ni mbuni multipurpose hahahhahaha, mnaogea hiyohiyo , mnafulia hiyohiyo ,mnaoshea vyombo hiyohiyo, mhhhhh kuoshea mabafu na magari je? nilisahau kumbe omo . tena anaweza kukuincourage akawa anakusifia kila siku unakuwa soft ukiogea omo....... weeee tena unabaki "MWE"😕!!!akidai ati nunua Ommo au mbuni ni multi purpose utajuuuuuta kuolewa nae baadae!
You single ladies out there, msiseme hamkuambiwa!
hahahahhahahaha WoS umenimaliza kabisaaaaa Mungu wangu kweliii mbona ni mbuni multipurpose hahahhahaha, mnaogea hiyohiyo , mnafulia hiyohiyo ,mnaoshea vyombo hiyohiyo, mhhhhh kuoshea mabafu na magari je? nilisahau kumbe omo . tena anaweza kukuincourage akawa anakusifia kila siku unakuwa soft ukiogea omo....... weeee tena unabaki "MWE"😕!!!