It's the life you chose.
Wote. Hao maarufu, na nyie mnaowasengenya na kueneza fitna.
Mimi kwa kweli nikifikiri sana, kuanza kumuongelea Le Mutuz na familia yake inakuwa ngumu.
Simjui kihivyo, kumsoma social media si kumjua, mambo ya familia mengi sana, na hata ningemjua ningeongea naye mwenyewe. Nisingekaanga mbuyu mitandaoni.
Siwezi kujipa umuhimu sana katika shauri nisilolijua, kumhusu mtu ambaye simfahamu, ambaye hata hajaniomba ushauri.
Kujipa umuhimu hivyo ni dalili ya emptiness katika maisha ya mtu. Ni kama vile mtu hana familia yake kuiangalia, hana kazi zake za kufuatilia, anaishia kuishi maisha yake kwa kumfuatilia Le Mutuz.
Yani mtu anakuwa na maisha empty mpaka anajitengenezea ukaribu wa kufikirika na Le Mutuz anajiona na yeye kama mwanafamilia wa familia ya Le Mutuz vilee.
Ni aina fulani ya emptiness.