Kupandikiza watoto chuki siyo kitu sahihi. Le Mutuz kwa hili anaonewa sana, namtetea

Kupandikiza watoto chuki siyo kitu sahihi. Le Mutuz kwa hili anaonewa sana, namtetea

Na hapa ndipo anapokosea Le mbebez, unajua ukisoma zile chats, Yule mtoto wa kike anaonekana ana maumivu Makali kuliko mtoto wa kiume. Na hii ni nature watoto wa kike wanapenda Baba zao kuliko wa kiume (refer Freud's theory).

Tena binti anaonekana Yuko tayari kuyajenga na Baba yake, na amemueleza kosa lake, amemueleza afanye nini Ili wawe Sawa....Ila ona alichojibu Le mutuz, anazidi kumshambulia msumari WA Moto eti marafiki zao ndo wamemtuma ayamalize na wao, 😳😳 so haitoki moyoni?

Ushauri wangu ni kwamba still ana nafasi Kwa huyo binti yake, ajishushe, apunguze ego isiyo na maana.

Kingine aachane na haya madrama na mapicha picha, watoto wa kike tuna wivu sana Kwa Baba zetu, aishi low key huku akitafuta maridhiano plus vizawadi. Yaani namhakikishia atakula bata maisha yake yaliyobaki hapa duniani. Aachane na madanga, Kwanza hawara hana shukrani.
 
Wewe umekuwa mmbea.

Ugomvi wa familia kati ya baba mama na watoto unaueneza mitandaoni.

Waache wenyewe wagombane kifamilia, watapatana kifamilia.
Inawezekana na wewe kuishi muda mrefu Marekani umeshapata American effect.

Waleeni Watoto wenu katika maadili ya Kitanzania.

Mimi Nina vianko vyangu vimezaliwa Marekani lakini vinaniamkia shikamoo.

Acha kutetea ujinga, tena huyo Neema hiyo kazi mpaka anakwenda Marekani ni influence ya Mzee Malecela na alipendelewa tu, hakuwa na sifa.
 
Yani ugomvi wa Familia mkagombanie Instagram? Halafu eti mediator ni Kigagula Mange Kimambi?

Sielewi kwa nini huoni makosa ya Neema kuleta hili swala kwa mtu ambaye ni enemy wa furaha za watu wengine?
Watanzania wengi kama wewe ni mabingwa wa kutoa ushauri ambao hawajaombwa, kwa watu wasiowajua, kwenye mambo ambayo hawayafahamu.

Wana nyege sana za kufuatilia mambo ya watu, wakati wao wenyewe mambo yao yamewashinda.

Hii inatokana na u busybody fulani wanaojipa, wanajipa umuhimu ambao hawana.

Wewe bila shaka unafurahia hizi habari, kwa schadenfreude.

Usingefurahia ungeona vibaya kuzisambaza.
 
Chanzo ni yeye mwenyewe
Mume au mke Ukimshindwa mwanamke au mwanaume hakikisha unawajibika kwa watoto wako. Uspofanya hivyo ndo hayo sasa

Ila nawaonea huruma hawa watoto maana washapoteza baraka zao toka Mungu. Baraka za Mungu zinapita kwa baba mzazi ndio zishuke kwa mtoto
 
Yaani wewe kaka lazima origin yako Ni Muha!yaani Kila kitu huwaga unabisha kila kituuu..halafu kila kitu unajua jamani huko ughaibuni Kuna Nini huko?
Hujakaa na mtu anayejitambua yuko wapi.

Hujaweza kujibu hoja kwa hoja kimantiki.

Ndiyo maana ukikutana na mtu anayejitambua kasimamia wapi, anaandika mambo kimantiki, kwa upeo wako mdogo kama wa guluguja asiye na ubongo wala uti wa mgongo, unamuita Muha.

Hata hujui kuwanyanyapaa Waha hivyo ni ukabila na tabia mbaya.

Umemnyanyapaa mpaka Makamu wa Rais wa nchi yako.

Hujui hilo.

Kwa sababu hapo ndipo mwisho wa upeo wako.
 
Chanzo ni yeye mwenyewe
Mume au mke Ukimshindwa mwanamke au mwanaume hakikisha unawajibika kwa watoto wako. Uspofanya hivyo ndo hayo sasa

Ila nawaonea huruma hawa watoto maana washapoteza baraka zao toka Mungu. Baraka za Mungu zinapita kwa baba mzazi ndio zishuke kwa mtoto
Unaijuwa child support Marekani? Sikia hivyo hivyo.
 
Chanzo ni yeye mwenyewe
Mume au mke Ukimshindwa mwanamke au mwanaume hakikisha unawajibika kwa watoto wako. Uspofanya hivyo ndo hayo sasa

Ila nawaonea huruma hawa watoto maana washapoteza baraka zao toka Mungu. Baraka za Mungu zinapita kwa baba mzazi ndio zishuke kwa mtoto
Wanawake Wana chuki tu mkishaachana kuwalisha sumu watoto hakukwepeki hata uwe unawapa milioni kila siku.
Hapa ni ishu ya maadili na sio uchumi.
 
Ila le mubebez amapaswa kubadilika sana. Ni mgonjwa yule lkn kila siku kujisifia yupo five star hotel namadem tofauti!

Kila siku ana madem tofauti na lazima awapige picha na kuwaleta insta kutamba!! Sijui anawalipa bei gn anawalala na kuwapiga picha wanakubali

Hivi mtu mwenye ugonjwa kama wake na umri huo ni wakuhangaika na madem kweli? Kila siku kujisifu yupo five star na mademu!!

Sina chuki nae ila inashangaza sana huyu mzee anazeeka vibaya
Kwa Yale matusi anayotukanana mitandaoni lazima Moyo umzingue tu.
 
Hujakaa na mtu anayejitambua yuko wapi.

Hujaweza kujibu hoja kwa hoja kimantiki.

Ndiyo maana ukikutana na mtu anayejitambua kasimamia wapi, anaandikq mambo kimantiki, kwa upeo wako mdogo kama wa guluguja asiye na ubongo wala uti wa mgongo, unamuita Muha.

Hata hujui kuwanyanyapaa Waha hivyo ni ukabila na tabia mbaya.

Umemnyanyapaa mpaka Makamu wa Rais wa nchi yako.

Hujui hilo.

Kwa sababu hapo ndipo mwisho wa upeo wako.
Nilijua tu utaniandikia waraka Kama wa mtume Paulo....
Sina haja ya kubishana na mbishi unaebisha kila kitu napenda tu kukuambia punguza kitu kujua...kila Uzi wewe ndio mbishi na unajua kila kitu aaaah sio poa
 
Back
Top Bottom