Sawa mkuu alichofanya huyo Mama sio sahihi na Kwa vile umeshakua ugomvi wa kifamilia,
Kiranga sio kwamba anatetea au kusema mambo Yako shwari, la hasha. Kama nimemwelewa vizuri na nnavyofikiria Mimi, tungewaachia wakapambana nalo wenyewe hukohuko.
Na kama kweli lengo ni kumfikishia ujumbe mwanachama mwenzetu wa JF, ungeweza kumwandikia peke yake nabila shaka angeona kweli Kuna Nia ya dhati ya kurekebisha na kukosoa Kwa staha. Lakini hii ya kuja kumwaga hapa ni kama umesaidia ipasavyo kazi ya hao hao unaowalaumu.
Mwisho wa siku hapa JF Kila mmoja ana mambo yake mengi na tuna watu wa kaliba zote na uchafu wa Kila aina, ukisema uhangaike na members wenzetu hapa utakuta unapoteza muda wako wa muhimu na usipate matokeo unayoyatakani Kwa hao watu.
Unatarajia kweli huyo Mama atabadilika Kwa huu Uzi?