Tunatofautiana namna ya kufikiri mkuu hasa hapo unaposema "wanamkalisha mtu miaka 8 ili uje umpe mtihani" kana kwamba elimu na ajira rasmi vina uhusiano wa moja kwa moja na nilazima iwe ni serikalini
Lengo la elimu ni kukutoa wewe tongo tongo uje upambane na mazingira yako ikiwemo ajira sasa hata ukikaa miaka 20 kuna shida gani
Yani mimi nisome la kwanza hadi chuo halafu nikipewa mtihani wa la kwanza nilalamike eti kisa ni miaka 12 toka nimalize la kwanza
Mimi nakuunga mkono unaposema wanachelewa kuleta usaili ili tuwahi kulamba asali au tuendelee na haso za kitaa ila interview na miaka ya kukaa kitaa bado havina uhusiano kabisa
Twende taratibu katika huu mfano wako
Mfano wako siyo relevant kwanini ??
Kwasababu huwezi fananisha mtihani wa la kwanza na wachuo ,, wote tunajua jinsi mitihani ya chuo ilivyo na vitu vingi na ndiyo maana hata wao sio wajinga kusema mtu asome per semister (miezi 4 tu ) na baad ya kuingia semister mpya vitu vya semister iliyopita havijirudii tena ask yourself why they don't repeat them ??
Lakini pia ,, time factor is also taken into consideration
Baada ya kumaliza miezi 4 tu wanakupa test ( U.E ),, tofauti na wanavyotaka kufanya utumishi
Tukirudi hata katika mfano wako wa mtiani wa la kwanza...... Kama mtihani wa la kwanza mtu atapewa baada ya miaka 10 mbele basi huo mtiani hautakuwa valid,,, kwanini ?? kwasababu hujazingatia time factor ( wewe ni mwalimu kasome zaidi test validity ,, factor that can affect test validity )
Mfano mzuri
Kuna askari polisi fulani hapa Tz alienda kufanya mtiani wa hesabu wa darasa la tatu pamoja na wanafunzi wa darasa hilo katika shule fulani ,, na mwalimu baada ya kusahihisha mitiani ile ukiwemo na mtiani wa askari polisi yule
Matokeo yalionesha askari polisi yule hakuna alichoambulja yani alipata sifuri kabisaa ,, wengi tulipoona clip ile mitandaoni tulicheka na kumkebei askari yule na kumuona hana akili
Lakin wengi tulisahau hii sababu ya time as one of the factor that can effect the validity of a test given to a student ,, yani kama ntakufundisha kitu leo afu nakuja kukupa mtiani wa hicho kitu nilichokufundisha baada ya miaka miwili mbele moja kwa moja huo mtiani hauko valid ..
Waziri Mkenda siyo mwalimu hivyo naweza kusema ndiyo maana kakurupuka kuingiza issue za interview kwa walimu na hoja yake ya kupata walimu bora ni hoja nyepesi mnoo aliyoitumia maana imeacha mashwari mengi kuliko majibu
Mfano why walimu bora je
- Ufaulu wa wanafunzi umeshuka??
- Wanafunzi huko madarasani hawaelewi kinachofundishwa ??
- Walikuwa wanachaguliwa na tamisemi siyo boraa ???
Na mengine mengi