Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Wewe jamaa achana na mambo mengi na kukariri vifungu.usifikiri watu hawajui yote hayo.hayo mambo sio bahati mbaya.hiyo ni michezo ya watu.hizo fault zinawekwa kimkakati tu.Uwezi kua na makosa yale yale miaka yote na hakunaga hatua zinazochukuliwa kwa wahusika.
 
Tumekwishaaaaaa🀣🀣
Usicheke inabidi kulia, kuombeleza na kugalala. Kuomba vyote vya kimataifa vichunguze mikataba yetu yote.

Ni kama tunapigwa mabomu makubwa kama kwenye ile hospitali gaza kila siku.

Mamia wanakufa kwa kukosa dawa, ajira, elimu, makazi. Wakulima wanateseka tu. Miaka sabini sasa.
 
Mimi hiyo Bilion 75 nimewaza sana...Inatosha kujenga mahospitali na mashule kadhaaa ila Dah acha bhna
 
Mkwere ni wa kunyonga au vipi? Sheria iwe retrospective wanyongwe[emoji2958][emoji2958][emoji2958][emoji2958][emoji848][emoji848][emoji2960][emoji2960]πŸ₯±πŸ₯±[emoji15][emoji15][emoji15]
 
Hapana lengo la kuweka hivi ni Kwamba a

Lengo la kuweka maoni haya sio kwamba sijui serikali wana think tanks wengi najua ila lengo langu ni moja tuu katika hawa wasomaji wa comments yupo mtu mmoja huenda akaja kuwa kiongozi au mtu mkubwa serikalini akaweza kuyafanyia kazi.
 
Hit them up.
Siyo bure Kuna uchafu mkubwa ....
 
To me, whether ilifufuliwa ili watu wapige pesa au la, issue ni kwamba kesi hii tuliingiaje? Kama tulikosea, hata kama si leo wala near future, lazima tulipe madeni..!!!

Wewe pamoja na Pascal Mayalla tujiulize yafuatayo.!!

1. Nani aliyetuingiza kwenye kesi??? Je ni aliyefufua kesi au aliyesababisha tuingie kwenye kesi..!??? Kwanini tunahangaika na aliyefufua badala ya aliyetuingiza kwenye kesi??

2. Huyo mfufua kesi, hadi awe na uwezo wa kuifufua na hatimaye kupata ushindi, hii kesi kusahaulika ndo kulikuwa pona yetu???

3. Kwani huko siku za nyuma hatukuwahi kuonywa na watu tofauti tofauti wakiwemo akina Lisu, Lema juu ya kesi za namna hii?

4. Kwanini kila wanaotuambia kuwa tunakoelekea ni kubaya huwa tunawaita siyo wazalendo?

5. Hao waliotuingiza mkenge leo, tunawafanya kitu gani?

6. Kulishawahi funguliwa mahakama ya mafisadi huko nyuma. To me, bila kupepesa macho wala kuumauma maneno, mahakama ile ilifunguliwa ili ku-deal na Lowasa tu. Yaani serikali nzima inahangaika na mtu mmoja. Matokea yake, na yeye jinsi anavyojua kucheza karata zake, akajiunga nao. Ndo ukawa mwisho wa mahakama ile. Hawa watu wanaotuingiza mkenge kila kukicha kwanini wasishitakiwe kwa uhujumu ujuchumi au ufisadi.??

7. Kuna watu kwenye almost kila deal la hela ambalo nchi yetu imepigwa wamooo..!! Yaani hao tukisema wameitia serikali mkononi tutakuwa tunakosea????

8. Mpaka hapo, kila tulilolipishwa kwa namna moja ama nyingine, lilishawahi semwa na baadhi ya watu, na nchi ikaweka masikio pamba. Kwa mtiririko huu, tuna mangapi tutalipishwa huko tuendako.??

TUACHE KUMPOTOSHA MAMA KWA KUMSIFIA KUWA ANAUPIGWA MWINGI WAKATI TUNALIPISHWA KILA SIKU KISA HAO HAO WANAMSIFIA KUWA ANAUPIGA MWINGI
 
Hii inji ni tajiri sana.. hivyo kuna baadhi ya viongozi wanaona kama hizo fedha ni zao hivyo wanaweza kuzifanyia lolote. Unajua tena tabia za maskini akipata kipato ( baadhi)

Tutawafanya nini, wanaamua kwa utashi wao na sio sheria na taratibu za kulunda mslahi ya nchi.

Hakuna cha ujinga, ni upumbavu tu.
 
Haikuwepo kivii na yule pofesa uchwara Mromo alikuwa anajibu kesi ipi?

Hii kesi Hii Hapa, jikumbushe:

 
Pascal Mayalla

Hii kesi kama serikali imeamua kuimaliza nje ya mahakama kwa $30 m, wamefanya la maaana sana kuliko wangeendelea kuvutana nayo, ilikuwa haina ushindi na wangelipa pesa nyingi sana na gharama kubwa kubwa za nenda rudi.

Hizi ndizo kesi alizotuumiza mwendazake na maprofesa wake uchwara kina Kabudi na Mruma.

Jikumbushe uone kama kulikuwa kuna ushindi hapa:



Aliyewashauri kulipa kwa kufikia makubaliano ya nje ya mahakama amefanya la maana sana.

Na mama kurishia, ia kafanya la maana na kaifanyia kazi R ya ya Reconciliation, nnauhakia na hapo hapo kaona fursa ya Resilience.

Hili ni la kupongezwa siyo kupondwa, hakuna aliyetupiga, tumejipiga wenyewe kwa sababu huwezi kurusha lawama kwa aliyeondoka.

SS to Reform na ku Rebuild.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…