Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Kupigwa billioni 75 ni ujinga au upumbavu? Tutaendelea kukubali kufanywa kichwa cha mwendawazimu hadi lini?

Hii kesi imefufuliwa na wanaume wapige pesa then maza wa mwambie anaupiga mwingi na majina mazuri mazuri huku wanapiga pesa za umma, umewahi kuona wapi kesi kubwa kama hii inaendeshwa kwa miezi 2? kuna kesi ya ubunge ambayo haina maslahi kwao leo ina miaka 2 haijulikani hata mwisho wake.
Wacheni uongo, ilikwisha lini? Hukumu yake iko wapi hapo ilipokwisha?
 
Lakini naona mwanga huko mbele. Baada ya kupoteza ile ya Nachingwea ambayo Prof Mruma alikuwa hajui cha kujibu, sasa Serikali imekubali ushauri wa settlement out of court. Maana zina sura moja zote
Aisee hii nchi hela tunazopotezaga kwa gharama ya maamuzi ya kukurupuka ya mtu mmoja au kwa sababu kuna watu wanakula 10% zrngekuwa zinaenda kwenye miradi ya maendeleo tungekuwa mbali sana.
 
Mungu akubariki Pascal Mayalla kwa kurudi kwenye uzalendo wa kweli tofauti na hapa kati ulipogeuka Chawa.

Inauma tena inahuzunisha tunavyotendewa
Hapa kapiga porojo nyingi lakini hakuna cha maana sana.

Hii kesi Serikali imeokoa kulipa pesa nyingi sana kwa kubali yaishe na walipe hizo tu.
 
Upinzani wakisema haya tunaitwa Vibaraka, hatujui! Hahahaaha sisi tumetangaliza siasa kwenye Kila kitu, siku tukiweza kutengenisha Kwa asilimia kadhaa tu tutakua mbali
Sasa kunalipi la maana hapa? Nyie semeni, mlitaka kesi iendelee mpaka lini?

Mnafahamu kila siku moja hii kesi na team inayokwenda nje ya Tanzania inatugharimu shillingi ngapi?

Kina Mruma wangekuwa wanaivuta tu kila siku ishe wajipatie [posho za bure, ndiyo akili zao zilipoishia.

Nyie hamkuona kesi mtu anakwenda hajuwi documents zake ziko wapi?
 
Nashukuru leo umeandika kama Paschal Mayalla, kimsingi hizi ni dili za Mkwere, hii kesi haikuwepo imefufuliwa mwezi wa 7 2023 September 2023 malipo yakafanyika sijui kwa budget ipi? Ukisikia wateule wanamsifia sn maza kupita MUNGU wao sababu ni dili kama hizi, mara awe Mama wa Taifa sijui Dkt huku nchi ipo gizani, hakuna maji petrol shida, majibu ni haya. Tuacheni uchawa tusimame na nchi yetu
Kuna watu hawana huruma kabisa na pesa za uma
 
Tujisahihishe kama ambavyo amewahi kuandika baba wa Taifa ili tusirudie makosa ambayo yatakuwa yanatugharimu kama Taifa.
Wakujisahihisha ni nani, Mruma au Kabudi?

Hii mikataba ya Kimataifa kujisahihisha kwake, siyo kuwaletea sheria mpya kila siku. Mkishaini nao kama kuna mabadiliko mkae chini muongee. Sisi tulifikiri Uris wa Tanzania una nguvu nje ya Tanzania.

Tulilewa madaraka na kubadili hovyo mikataba.
 
Itafutwe namna ya kuliwajibisha Bunge letu Tukufu lililotunga sheria batili na za ajabu, na kutufanya Watanzania wote tuonekane wajinga na wapumba...
Narudia,

Chagua kwa Umakini na Uangalifu 2025

CCM must go! Upo ulazima wa Chama changu kukaa pembeni na kujitafakari na kujitathmini. CCM inahitaji mapinduzi ndani mwake kabla haija leta Mapinduzi yanayohitajika Nchini. You must reform.

I second,
Bunge la 2025, turuhusu wagombea huru, ili watu independent wa maana wa kulisaidia taifa, wajitokeze
1000%
 
Hii inji ni tajiri sana.. hivyo kuna baadhi ya viongozi wanaona kama hizo fedha ni zao hivyo wanaweza kuzifanyia lolote. Unajua tena tabia za maskini akipata kipato ( baadhi)

Tutawafanya nini, wanaamua kwa utashi wao na sio sheria na taratibu za kulunda mslahi ya nchi.

Hakuna cha ujinga, ni upumbavu tu.
Dona kantri
 
Sasa kunalipi la maana hapa? Nyie semeni, mlitaka kesi iendelee mpaka lini?

Mnafahamu kila siku moja hii kesi na team inayokwenda nje ya Tanzania inatugharimu shillingi ngapi?

Kina Mruma wangekuwa wanaivuta tu kila siku ishe wajipatie [posho za bure, ndiyo akili zao zilipoishia.

Nyie hamkuona kesi mtu anakwenda hajuwi documents zake ziko wapi?
Wewe ni mpumbavu!
 
Pascal Mayalla

Hii kesi kama serikali imeamua kuimaliza nje ya mahakama kwa $30 m, wamefanya la maaana sana kuliko wangeendelea kuvutana nayo, ilikuwa haina ushindi na wangelipa pesa nyingi sana na gharama kubwa kubwa za nenda rudi.
Kwanza asante tena FaizaFoxy for this, ni kweli kukubali settlement out of court ya just US $ 30m out of US $ 100m, is a good deal, hoja yangu haya ni matokeo sio chanzo!. Wakati wapanga chanzo, wanayapitisha madudu yao Bungeni, tupo akina sisi tuliwauiza openly Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? humo tuliwaeleza the consequences ya sheria hiyo na tukawapa na mifano!. Leo tunapolipishwa, tunauliza waliosababisha hayo wako wapi na wamefanywa nini?.
Hizi ndizo kesi alizotuumiza mwendazake na maprofesa wake uchwara kina Kabudi na Mruma.
Usimuingize JPM kwasababu JPM sio mwanasheria, he is not expected to know this, kwa wenzetu wanapotunga sheria yoyote, pia wana focus on mitigation, watajishikia wapi!.

Ni kama kwenye IGA ya DPW na Bandari zetu, japo aliyesaini ni Prof. Mbarawa, amesaini kwa niaba ya Rais Samia, IGA ile ina mapungufu makubwa sana ya kisheria, kama nilivyo ya ainisha hapa Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! hatumlaumu Rais Samia, tunawalaumu wasaidizi wake!
Aliyewashauri kulipa kwa kufikia makubaliano ya nje ya mahakama amefanya la maana sana.

Na mama kurishia, ia kafanya la maana na kaifanyia kazi R ya ya Reconciliation, nnauhakia na hapo hapo kaona fursa ya Resilience.
Naunga mkono hoja
Hili ni la kupongezwa siyo kupondwa, hakuna aliyetupiga, tumejipiga wenyewe kwa sababu huwezi kurusha lawama kwa aliyeondoka
Nimekusikia!
SS to Reform na ku Rebuild.
Asante sana
P
 
Sasa kunalipi la maana hapa? Nyie semeni, mlitaka kesi iendelee mpaka lini?

Mnafahamu kila siku moja hii kesi na team inayokwenda nje ya Tanzania inatugharimu shillingi ngapi?

Kina Mruma wangekuwa wanaivuta tu kila siku ishe wajipatie [posho za bure, ndiyo akili zao zilipoishia.

Nyie hamkuona kesi mtu anakwenda hajuwi documents zake ziko wapi?
Kwahili, acha tukubaliane kutokukubaliana..!!

Soma na hii

Kwanza asante tena FaizaFoxy for this, ni kweli kukubali settlement out of court ya just US $ 30m out of US $ 100m, is a good deal, hoja yangu haya ni matokeo sio chanzo!. Wakati wapanga chanzo, wanayapitisha madudu yao Bungeni, tupo akina sisi tuliwauiza openly Zita Act Retroactively? Tutavunja Mikataba Yote Iliyopo? Can we Stand? Do we have the Guts? humo tuliwaeleza the consequences ya sheria hiyo na tukawapa na mifano!. Leo tunapolipishwa, tunauliza waliosababisha hayo wako wapi na wamefanywa nini?.

Usimuingize JPM kwasababu JPM sio mwanasheria, he is not expected to know this, kwa wenzetu wanapotunga sheria yoyote, pia wana focus on mitigation, watajishikia wapi!.

Ni kama kwenye IGA ya DPW na Bandari zetu, japo aliyesaini ni Prof. Mbarawa, amesaini kwa niaba ya Rais Samia, IGA ile ina mapungufu makubwa sana ya kisheria, kama nilivyo ya ainisha hapa Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! hatumlaumu Rais Samia, tunawalaumu wasaidizi wake!

Naunga mkono hoja

Nimekusikia!

Asante sana
P
Cha kufanyika ni kimoja tu, kwa kuwa sheria za Mikataba ya nje ya uwekezaji inalinwa kimataifa, kwa kuwa hata wakandarasi wa nje mikataba inalinsdwa kimataifa. Tuhakikishe kila mkataba gtunafata sheria za Kimataifa, tusikurupuke.

Kuna watu kama kina Habinder Singh na mwenzake yule mhaya, kazi yao kuvizia hizi kesi na kujipigia pesa tu. Wanajifanya wao ni ma lobbyists kumbe ni wapigaji tu.
 
Nashukuru leo umeandika kama Paschal Mayalla, kimsingi hizi ni dili za Mkwere, hii kesi haikuwepo imefufuliwa mwezi wa 7 2023 September 2023 malipo yakafanyika sijui kwa budget ipi? Ukisikia wateule wanamsifia sn maza kupita MUNGU wao sababu ni dili kama hizi, mara awe Mama wa Taifa sijui Dkt huku nchi ipo gizani, hakuna maji petrol shida, majibu ni haya. Tuacheni uchawa tusimame na nchi yetu
Yaani upumbavu wa MAGUFULI analaumiwa KIKWETE aisee hii nchi ina usenge sana.
 
Ingewachwa kesi iendelee yangekuwa matrilioni tena hatulipi kwa pesa za madafu. Waliokubali wayamalize nje ya mahakama na walipe hizo tu, wamefanya la maana sana.

Tutaendelea kulipa watu mpaka lini...? Wananchi wanataka waliohusika wawajibishwe hizo fedha za malipo sio mali yao ni kodi za watanzania
 
Ingewachwa kesi iendelee yangekuwa matrilioni tena hatulipi kwa pesa za madafu. Waliokubali wayamalize nje ya mahakama na walipe hizo tu, wamefanya la maana sana.
Tumefikia hatua ya kusifia kukubaliana nje ya mahakama yaani..!!! Siku zote ukiona mtu anataka makubaliano nje ya mahakama maana yake kaona anaenda kupigwa pakuwa ndani ya mahakama. Yaani ndani ya mahakama kwake ni kwa moto. Ni sawa na kuomba POOO...!!! Sasa Faiza wewe badala ya ku-deal na chanzo cha tatizo unahangaika na matokeo ya tatizo..!! Na ndo hapo panapokufanya useme AFADHALI hivi kuliko kesi kuendelea..!!

To me, walioshiriki wote wangefilisiwa tu..!! Uki-deal na wachache wengine wata - align acordingly
 
Back
Top Bottom