Kupitia UTT, Ninahitaji milioni 2 kila mwezi

Sema inflation rate ya tz imekaa kisiasa sana.

Sio ya kuiamini kabisa.
 
Asante mkuu,ila kuna swali nimekuuliza hapo kuhusu kuchukua mkopo na kuweka bank naomba unijibu kama hautajali
 
Mkuu una akili kubwa sana. Kama ninakuelewa hivi halafu baadae unanichanganya tena.
 
Asante mkuu,ila kuna swali nimekuuliza hapo kuhusu kuchukua mkopo na kuweka bank naomba unijibu kama hautajali
Unaweza ukachukua mkopo na kuwekeza kwenye bonds hata UTT Bond Fund na Liquid Fund pia mkuu. Chakuzingatia riba ya mkopo, inatakiwa iwe chini na ufanye long term investment ingawa ushauri mzuri ni kuwekeza kidogo kidogo kama ukiweza
 
Halafu mkuu nakuomba unisaidie mawasiliwano yako pm Kama hutojali.


Nimekupata Kuna jamaa hapa nikaongea naye hapa bank ananiambia kuwa unaweza kuta kila shilingi Mia unaweza ukawa unatoa ama unalipa 97.78tzs so bado na hapa Kuna value sijui ndio iyo unayosema capital gain
 
Mkuu una akili kubwa sana. Kama ninakuelewa hivi halafu baadae unanichanganya tena.
"Кто не рискует, тот не пьет шампанского" huu NI Mmoja wapo wa usemi wa kirusi ukimaanisha kwamba kama Huchukui Risk Maishani huwezi kukaa viti virefu na Kugonga Champagne. Risk kubwa niliochukua ni kuacha matakwa yangu ya uHacker, Nilianza lidigrii langu la Fundamental Informatics and Information Technologies, chuo kikuu cha Lomonosov Moscow state University , Huku nikipiga part time mambo ya Computation, Data science na Engineering nikiwa na Aim siku moja nitungue mashirika makubwa na kisha nikimbizie mpunga wote kwenye Crypto nkalale visiwa vya Bahamas hukoooo lakini ndo hvyo niliyabwaga yote nikawa Economic Hitman, Jasusi wa kiuchumi niliyetembea nchi nyingi na kukutana na maraisi wengi wa afrika ambao vichwa vyao ni mbumbumbu (IQ below 70).

Bhana Hiki chuo ndo chuo namba 1 kwa ubora nchini urusi, Bila mzee wangu kukazaa aiseee ningekuwaga UDSM pale na ningeishia hapo katikati lakini mungu mwema, sasa nakumbuka ile nafika fika urussi nilikutana na rafiki yangu mmoja wa kizambia manzi anaitwa francine , amekaa huko kama 3 years akawa ananipa michongo ya urusi yote ilivyo
stori ya makundi hatari ya Bratva ya huko urusi au sometimes wanaiita Orekhovskaya OPG , Opg ikimaanisha Organized Criminal Group. Stori nilizopewa ni kama shoti ya Ganzi mwamba niliogopa nkasema nitaweza.

Hii pisi nilitokea kuikubali sana, nikasema lazima nipite nayo so siku moja nkaorganize kamtoko! Sasa kuna karestaurant flani hv sio bei ghari kapo karibu na Lomonosov Moscow state University, kanaitwa marea restaurant naukumbuka mtaa ni Мичуринский пр. bhana kuna Lobster sio wa dunia Hii...... Kabla sijaendelea Hapa ndo kwa mara ya kwanza Nilipotekwa katikati ya Jiji la moscow na picha ya maisha yangu ikabadilika mpaka leo.

Чему́ быть, того́ не минова́ть.


Back to the Topic:
Mkuu sehemu gani nimekuacha nifafanue usije ukanipiga na nyundo? au Mzigo wa KQ? hapo nilimjibu kwa sababu alileta mambo ya cross currency kwamba unainvest in Bond may be za nchi nyingine au unainvest kwenye ma eurobonds huko so unakuwa exposed na Exhange rate risk na ili kuicover hii risk unapiga forward contract na mabenki lakini ina risk. Mfano KQ huwa nahedge mafuta ambapo alikosea hesabu ndo akapiga hasara ya bilioni 26 hukooo.
Mkuu wangu wapi nimekuachaaa. Ni DM kama kuna swala hujaelewa.
 
Ninashukuru kwa utayari wako wa kusidia. Taratibu nitaendelea kukuekewa.
 
Unazumzia vp kuhusu kushuka kwa thamani ya fedha katika kipindi hicho cha miaka 25. Fikiria ulinunua bonds za shilingi milioni 10 mwaka 98 halafu, pesa ambayo kwa kipindi kile ilikuwa na thamani sana ila unakuja kurudishiwa ileile 10m yako mwaka 2022.
 
UTT...nili nunua hisa nikiwa Form Six. Nika poteza cheti. Nilipo maliza chuo, nili fuatilia ili nijue Hisa zangu, niongeze hisa na niweze kuomba cheti kipya. Ila sikuweza kusaidiwa.
Nimepoteza Hisa zangu.
Kulikua hakuna account za online?
 
Account namba ya mfuko uliofungua unaikumbuka na pia umeharibu kufika makao makuu dsm
Hapo ndio shida mkuu. Nilikuwa Secondary. Cheti nikaweka home. Baada ya chuo na angalia cheti ili niongeze hisa. Cheti Hakuna duuh. Namba sikumbuki. Receipt ya malipo sina tena. Ni kaenda Posta angalau watumie majina yangu kunipata. Sikupata msaada. Japo nili anza na hisa ndogo, ila ningependa niendeleze Account Yangu.
 
20 yrs & 25 yrs bonds most utanunua kwa premium kwasababu ni hot cake. Refer ss&dd theories.

Ila zingine unaweza nunua kwa discount hata 10% sometimes depending on the demand of such bond.

Kwahiyo unatoa hata tsh 90 kwa bond ya tsh. 100. Na mwisho wa mkataba unqrudishiwa tsh 100 na sio tsh 90 ulillipa siku unanunua.
 
Unaongelea inflation. The same amount of money can not purchase the same quantity of goods 20 yrs later.

According to NBS & BOT, inflation ya Tz ni 4%. Ila bond ya 20 yrs unapewa 12.5% interest. Hapo una surplus ya 8.5%.

Na kwanini uwaze hela unayorudishiwa mwisho na usiwaze hela unayolipwa kila mwaka kwa miaka 25? Tena inakuwa mara 3 ya ile uliowekeza mwanzo.
 
Mkuu una akili kubwa sana. Kama ninakuelewa hivi halafu baadae unanichanganya tena.
hahaaaa....umenifurahisha mkuu, mimi pia namuelewa afu anafika mbele ananichanganya, ila kitu cha msingi nilichoolewa ni kuwa huu uwekezaji kwa treasury bills and bonds ni jambo zuri, lina faida... hii ndo point ya msingi niliyoipata, lakini pia nimeelewa kuwa unaweza kukopa kupitia viapnde ulivyo navyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…