Kupitia UTT, Ninahitaji milioni 2 kila mwezi

Kupitia UTT, Ninahitaji milioni 2 kila mwezi

UTT wanaalika members zao kwenye annual meetings pia. Hii PDF file niliyoambatanisha ni report moja wapo baada ya annual meeting ya mfuko mmoja wapo UTT. Ungeweza kuingia website ya UTT na kupata documents nyingi sana na zingejibu maswali yako mengi sana. Wapo wengi wanaobeza hapa lakini hawana ufahamu halisi wa mutual funds kama UTT ni kitu gani.

Jukumu la kujifunza unalo mwenyewe kwa kusoma vitabu, tafuta materials kwenye website husika, tembelea ofisi husika na uliza maswali, na mwisho wasiku utapata picha halisi ya kile unachotaka kukijua. Lakini hapa watakuja watu watakuambia mambo mawili matatu lakini kutokana na changamoto ya kwamba kuna watu wengine watakuja na kubeza bila kuwa na uelewa wa kutosha, utajikuta wewe unayumba.

Ningependa kuweka baadhi ya mambo sawa kulingana na nilivyoona comments nyingi humu.

1. Investment sio kitu sawa na biashara

2. Mifuko mingi ya UTT ina kua kwa compound interest rate >12% ambayo ni kubwa kuliko inflation rate ambayo ni kama 4%

3. Watu wengi wana mindset ya kufanya kazi/biashara na kupata income, wanaona kama investment na kutegemea the power of compound interest na kupata passive income ni uzembe.

4. Pesa unayotoa kwenye mfuko wako wa UTT haikatwi kodi, ila kwa baadhi ya mifuko wanakukata 1% as an exit load.

5. Watu wengi hawafikirii long term combined with the power of compound interest. Mfano vipande vya umoja fund mwaka 2005 vilikua TZS 100/kipande wakati saivi kipande ni kama 850 TZS/kipande. Sasa ni miaka 17 imepita. Fikiria mtu angekua amemuwekea TZS 3M (mwaka 2005) mwanae mdogo kwa ajili ya elimu ya juu. Mtoto anafika umri wa kwenda elimu ya juu leo(2022) angekua na kama TZS 24M, ambayo inatosha kumsomesha bila shida. Na bado sioni kama 24M ya leo ni sawa na 3M ya 2005, labda mimi sielewi inflation inavyofanya kazi, nileweshwe.

6. In a short term (one year, two years, few months) thamani ya vipande inaweza kuonekana imeshuka but in a long term, the graph is almost certainly going up!!
View attachment 2365037
Sema inflation rate ya tz imekaa kisiasa sana.

Sio ya kuiamini kabisa.
 
Hata usipoongeza vipande, interest inakuwa calculated on accumulated interest over time as well as on your original principal yaani original investment plus the income earned from investment ( can grow together/ zinakuwa pamoja). Jambo la muhimu wekeza then forget na uendelee na michakato mingine.
Asante mkuu,ila kuna swali nimekuuliza hapo kuhusu kuchukua mkopo na kuweka bank naomba unijibu kama hautajali
 
Mkuu we ni PM haina tatizo, Lakini ukianza kuongelea kuhusu mikopo ya Multi currency , hapo ni kuna changamoto na kunarisk mbalimbali za kuhedge mfano tu exchange rate rISK maana yake lazima uicover na forward contract. close look to impact ya kenya airways due to hedging failure A close look at the role of fuel hedging in Kenya Airways’ Sh26bn loss.

So nisiweke mambo mengi, what i wanted to say is "in a nut shell" wewe ni muajiriwa? upo kwenye vicoba? saccos? if theres a way u can get a loan/mkopo wa single digit interest mfano wafanyakazi wa mabenki wanakopeshwa hadi 5%, Saccos nyingine zinatoa 4 times amount uliyoweka plus 7% interest. unachofanya unaangalia tofauti kati ya TBond ya 25 years na Mkopo rate unayopewa , for example TBond 12.56 vs Saccos 7% difference 5,56% , so take the biggest amount utakayoweza kupata hata 1 Billion baba then nunua bond the interest + principal bond itajilipa bila wewe kufanya kitu baada ya miaka michache we ni mbuzi choma kwenye viti virefu.

Bond za kununua ni 20 na 25 Years tu ! PERIOD
So hakuna kununua bond zaidi ya hizo kama wewe ni retail, kumbuka LIQUIDITY ndo mpango mzima
Rejea: Buying 25 years Bond haimaaniishi ukae nayo miaka 25 unaweza nunua leo ukauza kesho... sasa kama ndo hyo why are u buying 10Y Tbond? Seriously.....
Mkuu una akili kubwa sana. Kama ninakuelewa hivi halafu baadae unanichanganya tena.
 
Asante mkuu,ila kuna swali nimekuuliza hapo kuhusu kuchukua mkopo na kuweka bank naomba unijibu kama hautajali
Unaweza ukachukua mkopo na kuwekeza kwenye bonds hata UTT Bond Fund na Liquid Fund pia mkuu. Chakuzingatia riba ya mkopo, inatakiwa iwe chini na ufanye long term investment ingawa ushauri mzuri ni kuwekeza kidogo kidogo kama ukiweza
 
Kwanini uhesabie thamani na bilioni 10 pekee na huesabii coupon rate unayopewa kila mwaka kwa 25 yrs?

Kwa case ya Tz;

Unatoa 10bn sometimes at a discount.

Coupon rate ni 12.56% kwa mwaka. Unalipwa kwa miaka 25.

Baada ya miaka 25 unarudishiwa 10bn yako wakati hapo kati umekula zaidi ya 31.4bn ya interest payements.

Yani 10bn yako baada ya miaka 25 unakuwa umeshapata zaidi ya 41.4bn.

Kama ulinunua kwa discount unaongeza capital gain.

Ni taahira pekee anaesema bond zinashuka thamani.
Halafu mkuu nakuomba unisaidie mawasiliwano yako pm Kama hutojali.

Nimekupata Kuna jamaa hapa nikaongea naye hapa bank ananiambia kuwa unaweza kuta kila shilingi Mia unaweza ukawa unatoa ama unalipa 97.78tzs so bado na hapa Kuna value sijui ndio iyo unayosema capital gain
 
Mkuu una akili kubwa sana. Kama ninakuelewa hivi halafu baadae unanichanganya tena.
"Кто не рискует, тот не пьет шампанского" huu NI Mmoja wapo wa usemi wa kirusi ukimaanisha kwamba kama Huchukui Risk Maishani huwezi kukaa viti virefu na Kugonga Champagne. Risk kubwa niliochukua ni kuacha matakwa yangu ya uHacker, Nilianza lidigrii langu la Fundamental Informatics and Information Technologies, chuo kikuu cha Lomonosov Moscow state University , Huku nikipiga part time mambo ya Computation, Data science na Engineering nikiwa na Aim siku moja nitungue mashirika makubwa na kisha nikimbizie mpunga wote kwenye Crypto nkalale visiwa vya Bahamas hukoooo lakini ndo hvyo niliyabwaga yote nikawa Economic Hitman, Jasusi wa kiuchumi niliyetembea nchi nyingi na kukutana na maraisi wengi wa afrika ambao vichwa vyao ni mbumbumbu (IQ below 70).

Bhana Hiki chuo ndo chuo namba 1 kwa ubora nchini urusi, Bila mzee wangu kukazaa aiseee ningekuwaga UDSM pale na ningeishia hapo katikati lakini mungu mwema, sasa nakumbuka ile nafika fika urussi nilikutana na rafiki yangu mmoja wa kizambia manzi anaitwa francine , amekaa huko kama 3 years akawa ananipa michongo ya urusi yote ilivyo
stori ya makundi hatari ya Bratva ya huko urusi au sometimes wanaiita Orekhovskaya OPG , Opg ikimaanisha Organized Criminal Group. Stori nilizopewa ni kama shoti ya Ganzi mwamba niliogopa nkasema nitaweza.

Hii pisi nilitokea kuikubali sana, nikasema lazima nipite nayo so siku moja nkaorganize kamtoko! Sasa kuna karestaurant flani hv sio bei ghari kapo karibu na Lomonosov Moscow state University, kanaitwa marea restaurant naukumbuka mtaa ni Мичуринский пр. bhana kuna Lobster sio wa dunia Hii...... Kabla sijaendelea Hapa ndo kwa mara ya kwanza Nilipotekwa katikati ya Jiji la moscow na picha ya maisha yangu ikabadilika mpaka leo.

Чему́ быть, того́ не минова́ть.

Back to the Topic:
Mkuu sehemu gani nimekuacha nifafanue usije ukanipiga na nyundo? au Mzigo wa KQ? hapo nilimjibu kwa sababu alileta mambo ya cross currency kwamba unainvest in Bond may be za nchi nyingine au unainvest kwenye ma eurobonds huko so unakuwa exposed na Exhange rate risk na ili kuicover hii risk unapiga forward contract na mabenki lakini ina risk. Mfano KQ huwa nahedge mafuta ambapo alikosea hesabu ndo akapiga hasara ya bilioni 26 hukooo.
Mkuu wangu wapi nimekuachaaa. Ni DM kama kuna swala hujaelewa.
 
Ninashukuru kwa utayari wako wa kusidia. Taratibu nitaendelea kukuekewa.
 
Kwanini uhesabie thamani na bilioni 10 pekee na huesabii coupon rate unayopewa kila mwaka kwa 25 yrs?

Kwa case ya Tz;

Unatoa 10bn sometimes at a discount.

Coupon rate ni 12.56% kwa mwaka. Unalipwa kwa miaka 25.

Baada ya miaka 25 unarudishiwa 10bn yako wakati hapo kati umekula zaidi ya 31.4bn ya interest payements.

Yani 10bn yako baada ya miaka 25 unakuwa umeshapata zaidi ya 41.4bn.

Kama ulinunua kwa discount unaongeza capital gain.

Ni taahira pekee anaesema bond zinashuka thamani.
Unazumzia vp kuhusu kushuka kwa thamani ya fedha katika kipindi hicho cha miaka 25. Fikiria ulinunua bonds za shilingi milioni 10 mwaka 98 halafu, pesa ambayo kwa kipindi kile ilikuwa na thamani sana ila unakuja kurudishiwa ileile 10m yako mwaka 2022.
 
UTT...nili nunua hisa nikiwa Form Six. Nika poteza cheti. Nilipo maliza chuo, nili fuatilia ili nijue Hisa zangu, niongeze hisa na niweze kuomba cheti kipya. Ila sikuweza kusaidiwa.
Nimepoteza Hisa zangu.
Kulikua hakuna account za online?
 
Account namba ya mfuko uliofungua unaikumbuka na pia umeharibu kufika makao makuu dsm
Hapo ndio shida mkuu. Nilikuwa Secondary. Cheti nikaweka home. Baada ya chuo na angalia cheti ili niongeze hisa. Cheti Hakuna duuh. Namba sikumbuki. Receipt ya malipo sina tena. Ni kaenda Posta angalau watumie majina yangu kunipata. Sikupata msaada. Japo nili anza na hisa ndogo, ila ningependa niendeleze Account Yangu.
 
Halafu mkuu nakuomba unisaidie mawasiliwano yako pm Kama hutojali.

Nimekupata Kuna jamaa hapa nikaongea naye hapa bank ananiambia kuwa unaweza kuta kila shilingi Mia unaweza ukawa unatoa ama unalipa 97.78tzs so bado na hapa Kuna value sijui ndio iyo unayosema capital gain
20 yrs & 25 yrs bonds most utanunua kwa premium kwasababu ni hot cake. Refer ss&dd theories.

Ila zingine unaweza nunua kwa discount hata 10% sometimes depending on the demand of such bond.

Kwahiyo unatoa hata tsh 90 kwa bond ya tsh. 100. Na mwisho wa mkataba unqrudishiwa tsh 100 na sio tsh 90 ulillipa siku unanunua.
 
Unazumzia vp kuhusu kushuka kwa thamani ya fedha katika kipindi hicho cha miaka 25. Fikiria ulinunua bonds za shilingi milioni 10 mwaka 98 halafu, pesa ambayo kwa kipindi kile ilikuwa na thamani sana ila unakuja kurudishiwa ileile 10m yako mwaka 2022.
Unaongelea inflation. The same amount of money can not purchase the same quantity of goods 20 yrs later.

According to NBS & BOT, inflation ya Tz ni 4%. Ila bond ya 20 yrs unapewa 12.5% interest. Hapo una surplus ya 8.5%.

Na kwanini uwaze hela unayorudishiwa mwisho na usiwaze hela unayolipwa kila mwaka kwa miaka 25? Tena inakuwa mara 3 ya ile uliowekeza mwanzo.
 
Mkuu una akili kubwa sana. Kama ninakuelewa hivi halafu baadae unanichanganya tena.
hahaaaa....umenifurahisha mkuu, mimi pia namuelewa afu anafika mbele ananichanganya, ila kitu cha msingi nilichoolewa ni kuwa huu uwekezaji kwa treasury bills and bonds ni jambo zuri, lina faida... hii ndo point ya msingi niliyoipata, lakini pia nimeelewa kuwa unaweza kukopa kupitia viapnde ulivyo navyo.
 
Back
Top Bottom