Bavaria
JF-Expert Member
- Jun 14, 2011
- 53,092
- 53,496
Sema inflation rate ya tz imekaa kisiasa sana.UTT wanaalika members zao kwenye annual meetings pia. Hii PDF file niliyoambatanisha ni report moja wapo baada ya annual meeting ya mfuko mmoja wapo UTT. Ungeweza kuingia website ya UTT na kupata documents nyingi sana na zingejibu maswali yako mengi sana. Wapo wengi wanaobeza hapa lakini hawana ufahamu halisi wa mutual funds kama UTT ni kitu gani.
Jukumu la kujifunza unalo mwenyewe kwa kusoma vitabu, tafuta materials kwenye website husika, tembelea ofisi husika na uliza maswali, na mwisho wasiku utapata picha halisi ya kile unachotaka kukijua. Lakini hapa watakuja watu watakuambia mambo mawili matatu lakini kutokana na changamoto ya kwamba kuna watu wengine watakuja na kubeza bila kuwa na uelewa wa kutosha, utajikuta wewe unayumba.
Ningependa kuweka baadhi ya mambo sawa kulingana na nilivyoona comments nyingi humu.
1. Investment sio kitu sawa na biashara
2. Mifuko mingi ya UTT ina kua kwa compound interest rate >12% ambayo ni kubwa kuliko inflation rate ambayo ni kama 4%
3. Watu wengi wana mindset ya kufanya kazi/biashara na kupata income, wanaona kama investment na kutegemea the power of compound interest na kupata passive income ni uzembe.
4. Pesa unayotoa kwenye mfuko wako wa UTT haikatwi kodi, ila kwa baadhi ya mifuko wanakukata 1% as an exit load.
5. Watu wengi hawafikirii long term combined with the power of compound interest. Mfano vipande vya umoja fund mwaka 2005 vilikua TZS 100/kipande wakati saivi kipande ni kama 850 TZS/kipande. Sasa ni miaka 17 imepita. Fikiria mtu angekua amemuwekea TZS 3M (mwaka 2005) mwanae mdogo kwa ajili ya elimu ya juu. Mtoto anafika umri wa kwenda elimu ya juu leo(2022) angekua na kama TZS 24M, ambayo inatosha kumsomesha bila shida. Na bado sioni kama 24M ya leo ni sawa na 3M ya 2005, labda mimi sielewi inflation inavyofanya kazi, nileweshwe.
6. In a short term (one year, two years, few months) thamani ya vipande inaweza kuonekana imeshuka but in a long term, the graph is almost certainly going up!!
View attachment 2365037
Sio ya kuiamini kabisa.