Duh! Kweli, ilianza kwa mdogo wangu wa kike kama homa ikampeleka siku tatu, ikahamia kwa wa kiume ikampeleka juu juu tuu, akaja jamaa jirani, then nikaipata, wote kwenye vipimo No malaria, No typhoid, wanaishia kusema UTI.
Kichwa kilianza kuuma, mwili unachemka ila joto halikupanda, niliharisha na kutapika, koo likauma na nilikohoa japo kidogo.
Hiyo yote ni kuanzia ijumaa mpaka jumatatu, baada ya hapo nikaanza kutohisi harufu wala ladha, nilichukua pilipili kichaa nilichohisi ni kuumia baada ya kuchubuka ulimi ila uhisi ukali.
Nilitumia Paracetamol kama pain killer, nilishauriwa pia kutumia Azuma kama antibotici ya kuzuia infection za bacteria kwenye mapafu just incase, kwa maana Covid-19 wakikukuta una lungs infection utaangukia pneumonia hiyo ndio worse.
Kutoka ile jumatatu mpaka ijumaa iliyofatiat pale ndo nikaanza kuhisi harufu kwa mbaali, tatizo lililobaki ni minyoo niliyokuwa nayo ikaanza kunifanya niwe nashindwa kula, nashukuru niliwahi dawa na sasa niko vizuri, namshkur mungu kwa kweli, hapo ndio nikaamini kwamba hii kitu ikikukuta na ugonjwa mwingine inakuwa zaidi, maana nilikuwa nahisi njaa ila nikila kidogo nahisi kutapika.
Zaidi:
Kuna rafiki zangu wawili, binamu yangu na jamaa wengine watano wamepatwa na hizi symptoms.
Nina kaka yangu ni MD yuko nje ya nchi ndio alinipa confirmation kuwa hizi ni dalili kubwa za Covid-19.
Cha kuzingatia:
1.Unaweza ukapona ila unawez ukakaa hata three weeks bado ukawa positive, so tuvae barakoa na sanitizer ili tusiambukize wengine
2.Pia kujikinga ili tusipate maambukizi tena, though wanasema body inatengeneza ka immunity ila sio very confirmed, ugonjwa ni mpya hypothesis ni nyingi.
3.Tuwatenge wazee na watu wenye matatizo ya kiafya kama kisukari, pressure etc.
4.Tusisubiri mpaka matamko ya serikali , tuzingatie na kufata utaratibu.
Mungu atulinde hili lipite.
Alexander The Great