Sehemu mbali mbali Duniani kumezuka mijadala ya watu wengi sana wakijadili tatizo la upotevu au ukosefu wa uwezo wa kunusa na kuhisi ladha ya chakula( Loss of taste and smell)
Kwa hapa Tanzania mimi ni mmoja wao na kuna rafiki yangu ni Dkt amenambia amekumbana na kesi nyingi hivi karibuni za wagonjwa wengi kulalamikia tatizo hilo.
Kitu kinachoacha maswali mengi ni kwamba Asilimia kubwa ya watu wenye virusi vya corona ndio hasa walioripoti tatizo hilo kwa wingi sana!
Sasa huenda wengi tumepatwa na tatizo hili lakini hatulichukulii kwa userious mkubwa.
Karibuni tujadili mbinu za kukabiliana nalo na kama ulishawahi kukumbana na tatizo hilo ruksa kushea!!
Sent using
Jamii Forums mobile app