Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Nilipata hilo tatizo baada ya kuvaa barakoa na mpaka sasa sivai barakoa nasikia harufu mwa mbaali na nilikua na homa kali lakin aada ya kujitibia malaria na uti ninajisikia vizur kwa sasa barakoa hazipo sawa wallah
Hata sanitaiza .....wengi wanalalamika kuumia kichwa
 
Hata wakijua hakuna cha kufanya huku kwetu!
Kama kungekuwepo na huduma bora za afya kwa huu ugonjwa ndio ingeleta maana,vinginevyo tegemea immunity yako tu ikuokoe.
Hivi mnajua nyinyi wote mna Corona?

Ila hamjijui?.na kuna watu watafikiri natania..

Kumbe Corona imesambaa hivi?
 
Hivi mnajua nyinyi wote mna Corona? Ila hamjijui?.na kuna watu watafikiri natania..Kumbe Corona imesambaa hivi?
Hili swali hukutakiwa hata kuuliza au kushangaa. Mbona maelezo yapo wazi tangu post namba 1 ? Au ulifikiri wanazungumzia nini?
 
Duh! Kweli, ilianza kwa mdogo wangu wa kike kama homa ikampeleka siku tatu, ikahamia kwa wa kiume ikampeleka juu juu tuu, akaja jamaa jirani, then nikaipata, wote kwenye vipimo No malaria, No typhoid, wanaishia kusema UTI.

Kichwa kilianza kuuma, mwili unachemka ila joto halikupanda, niliharisha na kutapika, koo likauma na nilikohoa japo kidogo.

Hiyo yote ni kuanzia ijumaa mpaka jumatatu, baada ya hapo nikaanza kutohisi harufu wala ladha, nilichukua pilipili kichaa nilichohisi ni kuumia baada ya kuchubuka ulimi ila uhisi ukali.

Nilitumia Paracetamol kama pain killer, nilishauriwa pia kutumia Azuma kama antibotici ya kuzuia infection za bacteria kwenye mapafu just incase, kwa maana Covid-19 wakikukuta una lungs infection utaangukia pneumonia hiyo ndio worse.

Kutoka ile jumatatu mpaka ijumaa iliyofatiat pale ndo nikaanza kuhisi harufu kwa mbaali, tatizo lililobaki ni minyoo niliyokuwa nayo ikaanza kunifanya niwe nashindwa kula, nashukuru niliwahi dawa na sasa niko vizuri, namshkur mungu kwa kweli, hapo ndio nikaamini kwamba hii kitu ikikukuta na ugonjwa mwingine inakuwa zaidi, maana nilikuwa nahisi njaa ila nikila kidogo nahisi kutapika.

Zaidi:
Kuna rafiki zangu wawili, binamu yangu na jamaa wengine watano wamepatwa na hizi symptoms.

Nina kaka yangu ni MD yuko nje ya nchi ndio alinipa confirmation kuwa hizi ni dalili kubwa za Covid-19.

Cha kuzingatia:
1.Unaweza ukapona ila unawez ukakaa hata three weeks bado ukawa positive, so tuvae barakoa na sanitizer ili tusiambukize wengine

2.Pia kujikinga ili tusipate maambukizi tena, though wanasema body inatengeneza ka immunity ila sio very confirmed, ugonjwa ni mpya hypothesis ni nyingi.

3.Tuwatenge wazee na watu wenye matatizo ya kiafya kama kisukari, pressure etc.

4.Tusisubiri mpaka matamko ya serikali , tuzingatie na kufata utaratibu.

Mungu atulinde hili lipite.


Alexander The Great
 
Mimi mwenyewe nimepitia hii hali ya kukosa kunusa.
Na mpaka sasa sijaanza kunusa harufu.
Asee omba usipate hii hali.kichwa kinauma.,nilihisi ni korona kabisa.
Nikawa nawaza sasa itakuwaje na nina familia na mtoto mdogo.?
Asee ni kushukuru MUNGU ..nashukuru famili.nashukuru kidogo kwa mbali naanza kunusa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unreported Covid19 cases
Wapendwa wenu(family) mmewakingaje? Baada ya nyie hawakuugua pia
Nimekuwa na utaratibu nyumbani kwangu.... kila siku tunatengeneza chai ya Tangawizi, kitunguu saumu, kitunguu maji, limao na asali tunakunywa nyumba Nzima. Nafikiri Ni zaidi ya wiki tatu sasa. Utaratibu huu upo.
 
Wakuu Kichwa cha Habari Kinajieleza.

Nina takriban wiki na siku 2 Sasa Nimepoteza uwezo wa kunusa na taste, yani hata harufu ya perfume sihisi kitu.

Najua humu Jf, tuna wataalam na wajuzi wa mambo,watatusaidia tiba na ushauri pia.

Karibuni wataalam.

Sent using Jamii Forums mobile app
===


Mkuu hiyo ni KORONA.
ANZA KUPAMBANA MAPEMA PIGA MALIMAO NA TANGAWIZI MIXTURE ITAKUSAIDIA BILA KUSAHAHU KUJIFUKIZA.
 
Me niliumwa February mwishoni. Baada ya Mimi kuumwa aliumwa bibi yangu wa umri wa miaka 85. Vichomi kifuani, mafua makali, kukosa ladha ya kula, kuhisi joto kali, kichwa kuuma sana, na kushindwa kupumua.... Nilichoma power cef 2 kila baada ya masaa 24 kubanwa kukapungua Hadi Hali hii ikaisha yenyewe mdogomdogo. Nilijua ni pneumonia.
Asante Mungu
 
Mimi walipotangaza case ya kwanza ya corona tu nikamchukua mama nikampeleka kijijini huko, nikajihisi nina roho mtakatifu na magonjwa yake ya uzee, maana haikunichukua wiki tatu tu, mnyama corona akaniingia, kanisumbua sana. nikapambana naye kimya kimya, nashukuru Mungu niko ok now, nikafikilia, what if ningekuwa na Mama hapa nyumbani.
 
Mimi walipotangaza case ya kwanza ya corona tu nikamchukua mama nikampeleka kijijini huko, nikajihisi nina roho mtakatifu na magonjwa yake ya uzee, maana haikunichukua wiki tatu tu, mnyama corona akaniingia, kanisumbua sana. nikapambana naye kimya kimya, nashukuru Mungu niko ok now, nikafikilia, what if ningekuwa na Mama hapa nyumbani.
Duuh pole mkuu
 
Mimi walipotangaza case ya kwanza ya corona tu nikamchukua mama nikampeleka kijijini huko, nikajihisi nina roho mtakatifu na magonjwa yake ya uzee, maana haikunichukua wiki tatu tu, mnyama corona akaniingia, kanisumbua sana. nikapambana naye kimya kimya, nashukuru Mungu niko ok now, nikafikilia, what if ningekuwa na Mama hapa nyumbani.
Mkuu ulipona baada ya mda gani ninaumwa mbavu na kifua mafua mepesi, homa iko juu kikohoz kikavu nikikohoa mbavu zinauma,,, kichwa hakipoi aiseee nimechoma sindano za mishipa kifua kinaendelea vzur
Imebaki homa na kichwa
Mme wangu yeye hasikii harufu anawiki Sasa
bint yetu yeye anamafua
 
navosoma hizi comments naanza kuamini huyu mdudu anaweza kuwa alipita nyumbani. mimi naishi na wazee wangu wiki kama mbili zilizopita bi mkubwa aliumwa sana hospitali kupima hamna kitu ila UTI kidogo. ikawa ni mwendo wa homa kali usiku na kukohoa sana tukawa tunamweke maji ya moto yenye limao nyingi anajifunikiza. tukaanza kunywa chai ya malimao mengi na tangawizi nyumba nzima, mchana tunakunywa juice ya ubuyu mix na rosella/choya. bi mkubwa kapona karudi hali ya kawaida mzee akaanza kuumwa jumapili kwenda hospitali hamna kitu. yeye hana homa ni kukohoa na mwili kuchoka. jana kaanza kuwa na nguvu. dada yangu kuna siku alilalamika nimuonjee mboga hasikii kitu basi ikapita. binafsi sijaona chochote naamini ni Mungu tu anatusaidia hivo hivo.
 
Back
Top Bottom