Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Niliona kama nakufa vile,mwili ukawa kama umepondwa na mawe,
nabanwa ndani kwa ndani macho yanatoa machozi tu,
harufu hata ya chooni sisikii..
mliopitia haka kaupepo poleni naelewa shida zake
Mi jana niliamka mchana na viungo vikawa vinauma hatari na usiku sikulala but leo nimepata nafuu ila tatizo la kutohisi ladha na harufu limeanza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilipata same issue. Kuanzia leo nimeanza kupata harufu na ladha.

Imenipa shida sana asubuhi kunusa nguo ili nijue kama chafu au safi. Maana me nguo uwa nanusa kwanza ndio navaa. Week izi mbili nikawa natupia tu bila kujua harufu yake.

Fanya mazoezi mzee, otea jua na Maji sana ya moto na chai.
Hii tabia ninayo,navaa nguo zaidi ya mara moja,nainusa kama haina arufu ya jasho itarudiwa,ikiwa na harufu ya jasho hata kwa mbali hio ni chafu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu, hukupata constipation kwa aina hii ya mlo??
Acha tu mkuu... Mdomo unakuwa kama umepigwa ganzi, kama kidonda ndugu hv.
Sometimes unaweza kumlaum mpishi wa chakula hajatia chumvi kumbe hapana,
Nimewahi kula chapati + maharage wiki 3 mfululizo asubuhi+mchana+usiku maharage yenye pilipili nyingi ndio nilipenda chakula cha namna hii.. sikuwa na hamu ya chakula tofauti na hiki karibu mwezi mzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilijaribu kutafuna hadi pilipili kichaa ndo nikawa nasikia kamuwasho kwa mbaliii, na limao ndo nahisi ladha kwa mbaliii, hii ni baada ya kupitia changamoto zifatazo; kuumwa kichwa kusikoeleweka yaani kichwa kizito tuu, kichomi, mgongo kuuma, misuli, kikohozi, mafua yasiyoeleweka yaani pua haikuziba. Matibabu niliyo tumia.ciproflaxin dozi, orodar,ampiclox dozi, metro dozi, brufen, limao, tangawizi,kitunguu sahumu, juice ya ukwaju, juice ya pera, peasi.
Baada ya kupata nafuu nikabaki na hii dalili chakushangaza leo wamekuja kunyonya choo jirani kila mtu analalamika harufu nawashangaa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app

Elimu dhidi ya huu ugonjwa wa Corona inapaswa kusambazwa..
Inaonekana umewagusa wengi Sana bila kujua
 
Elimu dhidi ya huu ugonjwa wa Corona inapaswa kusambazwa..
Inaonekana umewagusa wengi Sana bila kujua
Hizo dalili alizozitaja mtoa mada mm nimezipitia zote kwa wiki mbili mfululizo,nikatumia sana tangawizi na limao(juice) ogopa sana kutopata radha ya chakula aisee mm ni mpenzi mkubwa sana wa wali samaki lkn wiki mbili hizi nilikuwa naona Kama matope,nilijilazimisha kufanya jogging km 12 kila siku jioni mpaka nimepona,ajabu nikitoka jogging nikivua nguo tu nahisi baridi Kali mpaka naoga maji ya baridi nakubali hii CORONA inakuja kwa njia nyingi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kama ni corona basi kwa dalili za hawa basi bongo wengi watapona au haina nguvu
Elimu dhidi ya huu ugonjwa wa Corona inapaswa kusambazwa..
Inaonekana umewagusa wengi Sana bila kujua
 
Sasa kama ni hivo si ni kama mafua tu,maana hapa hamna anayeonyesha imemtesa sana kama tunavyosikia inatisha
Hizo dalili alizozitaja mtoa mada mm nimezipitia zote kwa wiki mbili mfululizo,nikatumia sana tangawizi na limao(juice) ogopa sana kutopata radha ya chakula aisee mm ni mpenzi mkubwa sana wa wali samaki lkn wiki mbili hizi nilikuwa naona Kama matope,nilijilazimisha kufanya jogging km 12 kila siku jioni mpaka nimepona,ajabu nikitoka jogging nikivua nguo tu nahisi baridi Kali mpaka naoga maji ya baridi nakubali hii CORONA inakuja kwa njia nyingi sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii ni dalili ya CORONA KABISA HATA MIMI NDIO INAISHIA ISHIA DAAH CORONA NUX SANA AISEE..

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hivi mnajua nyinyi wote mna Corona?

Ila hamjijui?.na kuna watu watafikiri natania..

Kumbe Corona imesambaa hivi?
Very true mkuu hizi ni dalili za Corona kabisa ila watu wanadhani ni zile dalili za kukohoa na mafua....kwa sasa wengi inakuja kwa kupoteza ladha na harufu plus viungo na homa sometimes
 
Back
Top Bottom