Nilipitia hii hali hii week nzima aisee mafua makali kichwa kuuma mbavu zinabana sisikii radhaa ya chochote mgongo unauma usiku nikawa naamka nakaaa tu kikiuma hichi kinaacha kinaanza kuuma kingine.baaadaye nikaanza kohoa kifua kikavu hakiishi.nipo mkoa kikazi ikabidi nipige simu na kuwaambia mwenzenu sijui kama nitatoboa piga simu kwa watu wangu wa karibu woteee.ikabidi nitafute limao na tangawizi ndio ikawa pona yangu.huu ugonjwa unatesa aisee pumzi inakata ukivuta hewa mapafu yanauma daaaah asante Mungu