Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Kupoteza uwezo wa kunusa yaweza kuwa/ni dalili za mwazo za COVID19

Tuendako hali itakuwa mbaya sana, maelezo ya tiba walizotumia yaweza saidia wengi kuepusha mafuriko ya wagonjwa hospitalini. Kipupwe huwa na upepo unaotimua vumbi kali na kila nyumba vikohozi na mafua haviponi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivi mnajua nyinyi wote mna Corona?

Ila hamjijui?.na kuna watu watafikiri natania..

Kumbe Corona imesambaa hivi?

mimi sikuhutaji kipimo kinothibitishie kwamba nilikua na corona, nilipopata dalili direct nikajua nima corona, imenipelekesha 2weeks na nawajua wengi tu wenye hizo hali na wamepona wengine
 
Dah Corona hiyo tena ni mbaya sana inaweza kusababisha stroke!
Mi mbona nilianza kula aspirin Kama Sina akili,action kila baada ya masaa 4,Hadi maumivu ya kwenye roho yakapotea
 
Sehemu ninapofanyia Kazi karibia watu 10 wote tulipata hiyo changamoto.. Kupoteza uwezo kupata ladha na kunusa harufu yoyote..

Ukipitia machapisho mbalimbali katika mitandao inayo aminika kama Medscape.. Hali hiyo ni ishara kwamba umepata maambukizi ya CORONA (mild) siyo maambukizi yale makali na sasa upo katika "recovery stage" kwa maana kinga yako ya mwili imeweza kupambana na maambukizi hayo.

CORONA ipo na wengi tumepata maambukizi kiasi kwamba naamini muda si mrefu tutapata ile "herd immunity" na ugonjwa utakuwa dormant... Ila tutapata shida sana maana sio kila mtu atapata hiyo bahati ya kupona hayo maambukizi kwa kuwa na kinga imara.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tarehe 27/4 nillienda kupima malaria/homa kipimo kikasoma NO PARASITES huku nasikia dalili zote za homa..

doctor akaniambia niondoke nikajisikilizie

harufu na kukosa ladha bado vipo
 
Sasa kama ni hivo si ni kama mafua tu,maana hapa hamna anayeonyesha imemtesa sana kama tunavyosikia inatisha
Mkuu corona ni clinical finisher,Kama haupo ndani ya kumi na nane haina shida sana,Ila jisikie hivyo harafu kasalimie wazee wako Kama wanaumwa umwa,ndo utajua Covid- 19.Wewe unadhani magu haipendi Dar?
 
Sehemu ninapofanyia Kazi karibia watu 10 wote tulipata hiyo changamoto.. Kupoteza uwezo kupata ladha na kunusa harufu yoyote..

Ukipitia machapisho mbalimbali katika mitandao inayo aminika kama Medscape.. Hali hiyo ni ishara kwamba umepata maambukizi ya CORONA (mild) siyo maambukizi yale makali na sasa upo katika "recovery stage" kwa maana kinga yako ya mwili imeweza kupambana na maambukizi hayo.

CORONA ipo na wengi tumepata maambukizi kiasi kwamba naamini muda si mrefu tutapata ile "herd immunity" na ugonjwa utakuwa dormant... Ila tutapata shida sana maana sio kila mtu atapata hiyo bahati ya kupona hayo maambukizi kwa kuwa na kinga imara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mi toka jana ndo imeanza iyo hali ya kutosikia harufu au ladha yoyote na pia kuna kitu kama kimekwama kooni

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Niliona kama nakufa vile,mwili ukawa kama umepondwa na mawe,
nabanwa ndani kwa ndani macho yanatoa machozi tu,
harufu hata ya chooni sisikii..
mliopitia haka kaupepo poleni naelewa shida zake
Hii hali niliipitia mwezi Januari 2020!
 
Nilipata hilo tatizo baada ya kuvaa barakoa na mpaka sasa sivai barakoa nasikia harufu mwa mbaali na nilikua na homa kali lakin aada ya kujitibia malaria na uti ninajisikia vizur kwa sasa barakoa hazipo sawa wallah
 
Nilijaribu kutafuna hadi pilipili kichaa ndo nikawa nasikia kamuwasho kwa mbaliii, na limao ndo nahisi ladha kwa mbaliii, hii ni baada ya kupitia changamoto zifatazo; kuumwa kichwa kusikoeleweka yaani kichwa kizito tuu, kichomi, mgongo kuuma, misuli, kikohozi, mafua yasiyoeleweka yaani pua haikuziba. Matibabu niliyo tumia.ciproflaxin dozi, orodar,ampiclox dozi, metro dozi, brufen, limao, tangawizi,kitunguu sahumu, juice ya ukwaju, juice ya pera, peasi.
Baada ya kupata nafuu nikabaki na hii dalili chakushangaza leo wamekuja kunyonya choo jirani kila mtu analalamika harufu nawashangaa tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hio ndio Covid 19. Bila kupepesa..
Endelea na matibabu ndugu yangu na walinde wengine
 
Nna hakika mpaka sasa nusu ya watanzania tushaumwa na robo wamepona na wengine rovo wapo katika revovery stage
 
Back
Top Bottom