mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Leo Baraza Kuu la Umoja wa Màtaifa lilipigia kura azimio lililopendekezwa na Marekani kuiondoa Urusi kwenye tume ya hàki za binadamu ya umoja wa mataifa.
Sababu ni Urusi kudaiwa kukiuka haki za binadamu ñchini Ukraine wanakopigana vita.
Katika kupiga kura Tanzania iliamua kuungana na nchi zingine 58 kugomea kura hiyo (kutokupiga kura).
Nchi zilizogomea kura zimo India, Afrika ya kusini, Brazil, Bangladesh nk. Zilizopiga kura kupinga azimio zipo 24 ikiwemo Urusi, China, Korea kaskazini, Cuba, nk.
Zilizopitisha azimio zipo 93 ikiwemo Marekani na nchi za Magharibi.
Japo azimio limepita lakini dunia imegawika katikati. Wale ambao hawakuunga azimio kwa maana ya kulipinga au kuligomea nchi zao zina watu wengi zaidi kwa kuwa zimo India, China, Brazil na Bangladesh zenye watu wengi zaidi.