Kusema ukweli mtaani hali ni mbaya, cha kushangaza viongozi hawajali kabisa

Kusema ukweli mtaani hali ni mbaya, cha kushangaza viongozi hawajali kabisa

Mi nimelia sana usiku nikitaman hata mchoz wangu ugeuke pesa nizikute asubuhi ndo kwanza nimekuta mto umeweka alama.Na shule ndo hizo zinafunguliwa j3[emoji53][emoji36][emoji24]
Dah kweli January imekuwa mwezi mfupi sana
 
Hali ni mbaya hali ni mbaya kupita maelezo, mitaani hali inazidi kuwa tete vitu havishikiki bei nashangaa imekuaje kumekua na mfumuko wa bei za bidhaa wa ghafla namna hii? yani vitu vimepanda bei kwanzia dawa ya mswaki mpaka vifaa vya kielekroniki na vifaa vya ujenzi,

mfumuko wa bei huu unatuathiri sana cha kushangaza viongozi ni kama vile hawajali hii kitu wanaona ni kawaida tu wako bize kutafutana kwaajili ya uchaguzi wa 2025, ajira hakuna, kazi hakuna hela hakuna vitu vinapanda bei hovyohovyo.

nyie viongozi mnajua kua Raia wenu sasa hivi hata chai hawanywi? na mboga tunapika bila mafuta.

inahuzunisha sana asee tunaishi kama digidigi

View attachment 2079053
Huku kwetu vijiwe vya kahawa vinapungua uwepo wa MAFUNDI WAASHI kukaa bure....

Mama ameifungua nchi na zile trilioni 1.3 tunaziona wenzako....
 
Ushauri tu: ada binafsi huwa nalipa novemba kwa ajili ya mwaka ujao...hapa niko mwepeesii...ada ni stress sana ya kuanza nayo mwaka usipoweka mipangilio yako vizuri....hapa niko kutafuta ada ya muhula wa pili nilipe mwezi wa pili niwe sina deni la ada ya 2022....tuweke mipangilio kulingana na nafasi ya kiuchumi tuliyomo tutapunguza stress.
Hii nzuri
 
Mama keshasema mbuzi wale ila wasivimbiwe [emoji2297]
 
kwa mfumko wa bei ulivyo kwa sasa ni heli Mungu aturudishie yule dikiteta wetu tu,maana hawa wanademokrasia watatua kwa ukimya wao huku bidhaa mitaani hazishikiki bei.
 
Tofauti iliopo sasa na awamu ya tano ni kwamba awamu ya sita tunaishi bila hofu kutoka juu ila kiuchumu awamu ya sita aliharibu sanaa paka mda upite
Pambana hakuna awamu rahisi.Magufuli mlisema amebana,kafa mkanywa na pombe kufurahia,leo tena bado mambo mnadai ni magumu.na bado

Hakuna awamu rahisi,fanya kazi
 
kwa mfumko wa bei ulivyo kwa sasa ni heli Mungu aturudishie yule dikiteta wetu tu,maana hawa wanademokrasia watatua kwa ukimya wao huku bidhaa mitaani hazishikiki bei.
Yaaani mliomba Magufuli atoke,saiv mnaomba tena arudi,Mungu si wakumgeuza geuza akili hivyo km unavykfikiria.mtalimia meno 😂😂
 
Kg ya viazi mbatata mkoa naoishi imetoka shs 800 hadi 1500
 
Mfumuko wa bei wa 100% umetokea kwenye nini na katika miezi ipi??
 
Back
Top Bottom