Kushabikia Polisi kuua watuhumiwa, ni ujinga uliopitiliza

Asilimia kubwa polisi huwajua wahalifu aisee,
Maana kwenye hii operation vijana wengi wamekamatwa , Mimi namfano mtaani kwetu kuna baadhi ya vijana walikamatwa lakini hakuna hata mmoja aliyeuwawa waliishia kunyolewa nywele za viduku na virasta uchwara kisha wakaachiwa
 

Una maana waliyowafanyia kina Ben, Lijenje, Azory, Lissu au hata wale wa kwenye viroba ni sawa kwa sababu wao ni malaika?
 
Nimekusoma mkuu. Kumbe hapa hoja ni kwamba wanaokamatwa bado ni washukiwa mpk watakapothibitika na kutiwa hatiani .
 
Mimi sikatai Polisi wanajua wahalifu mitaani...
Nchi hii ina usalama wa Taifa....
Nchi za nje wanawapeleka magereza ya kilimo na ufugaji miaka hata 10...

Unajua mtu ni nguvu kazi ya Taifa sio kuuwa nguvu ...
Unampeleka maximum security prison.... Kilimo tuu na ufugaji...

Nchi inapata mazao... Products zinaongezeka... Nk nk... Na baada ya miaka 10 anaajiriwa huko huko kuwasimamia watakaoletwa wengine...

Maisha yanaendelea
 
Una maana waliyowafanyia kina Ben, Lijenje, Azory, Lissu au hata wale wa kwenye viroba ni sawa kwa sababu wao ni malaika?
Nyie mnaojifanya watetezi Wa haki za binadam ndio mnaofanya raia wema tuishi kwa tabu kwa kuhofia watu ambao hawana huruma na RAIA wenzao , imagine MTU anakuja na panga anakuchanja Kama kuni alafu leo kakamatwa unaanza kumtetea aisee watu Kama nyie hamfai kabisa yaani mnatetea wahalifu , sikubaliani na nyie hata kidogo ,

Ukiua kwa upanga na wewe utakufa kwa upanga
 
Extrajudicial killings ni kinyume na Katiba yetu ya Tanzania.

Kamata Vibaka wapeleke Mahakamani.
Mahakamani kufanyaje? Kuna watu katika jamii lazima waondoke duniani kuwe salama, mm binafsi ningependekeza JWTZ wangehusika katika hii operation kama Kibiti na isingerudia milele
 
Nimekusoma mkuu. Kumbe hapa hoja ni kwamba wanaokamatwa bado ni washukiwa mpk watakapothibitika na kutiwa hatiani .

Kutokea Tarime tunaendelea kusikilizia nini kiliwapata Washukiwa wanne wale.

Dhahiri shujaa wenu mnayempongeza ndiye mtuhumiwa Numero uno!

Disgusting.
 
The end justifies the means....Acheni uhalifu,mtakwisha kama mlivyomaliza wenzenu.
 

Una uhakika hawa waliouwawa wamechanja watu kama kuni?

Pande za Tarime Kuna ushahidi kuwa tuhuma zako si za kweli.

Ushahidi wa maovu ya polisi kuanzia lini mmekuwa wageni nao?

Kwanini kama ni halali kuuwa watuhumiwa huu wigo usipanuliwe Ili kuwashughulikia wahalifu wote au hata kuidhinishwa tu kuwa halali kwa mujibu wa sheria?

Tangu lini makosa mawili yakahalalisha jingine?
 
Mtoa uzi taarifa zako tumeshazipata, wewe ni kibaka panya road, endelea kukaza ila wenzio wameshakutana na mkono wa chuma. Chunga sana
 
Mtoa uzi taarifa zako tumeshazipata, wewe ni kibaka panya road, endelea kukaza ila wenzio wameshakutana na mkono wa chuma. Chunga sana

Kwa macho yako yalivyo juu juu kwani inahitaji hata taarifa? Kama ungali mzima wewe hiyo mbona ni bahati mbaya mno!
 
dawa ya muhalifu anaye tumia silaha ni kifo tu maana ukichelewa anakuuwa wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…