Habari Wana MMU,
Naomba kuuliza Wanawake wenzangu,
Nilimuona Shogangu kasuka zile nywele za kimasai nikazipenda sanaa
sasa nikasema niende na kwakweli sijasuka nna miaka kama 10 sababu mr Hataki
This time nikamuomba akakubali baada ya miaka 10 ilikua kama bahati..
Kwakua nyewele zangu ndefu sikuhitaji rasta zakuongezea,haya shosti akanipitia
J"pili tukaenda kufika macho yakanitoka kumbe wasusi wanaume wa kimasai
nikamuliza mbona wanaume kasema ndio wanaojua wacha ushamba wako
haya akaongea nao nikaanza kusukwa mmmmm wamenizunguka Wamasai wa 5
sasa ule mkao wao yani wanakugusa na madudu yao huyu na wako busy kuongea kikwao
sielewi wanasema nini,shoga nae hayupo,mbaya zaid vikoi vyao vinanuka hatari,
nilistahmili kama nusu saa cm yangu ilipoita nikawambi waniache, nilipomaliza cm nikawambia
ntarudi baadae nikatoa elfu 20 nikasema nakuja waendele na mteja mwengine mpaka nikirejea
sikurejea tenaa...
Sasa niulize wadada mnaosuka ivi hii imenitokea mimi tuu au hawa wamasai ndio TABIA YAO?