Huu uzi ni wa kujitukana na kijichukia kama Mwafrika. Ni wa kukubali ubaguzi wa RANGI na falsafa za kina Hitler.
Duniani kuna watu wenye njaa kali na mateso ya ufukara kama Korea ya DPRK? Kama Iran ni peponi mbona Wairan wengi wanakimbilia nchi za Ulaya kwa Wakristo ambapo Ukristo haukubaliki huko kwao Iran.
Kutengeneza silaha za maangamizi kila nchi ikiamua inaweza kmf silaha za kibaiolojia kama COVID-lengo si kuteketeza binadamu.
Acha kukalili Iran atengenezi silaha tu.
Mkuu ngoja nikupe sifa chache tu za Iran.
(1)Iran ndo taifa la pili kwa nguvu za kiviwanda katika eneo la mashariki ya kati na Asia magharibi baada ya Uturuki.
(2) Iran ni mtengenezaji mkubwa wa magari ambapo huwa inayauza mashariki ya kati, Asia Magharibi,na Asia ya kati na baadhi ya nchi za ulaya mashariki.
(3)Madawa na vifaa tiba vyote ambavyo vina tumika ndani ya Iran asilimia 80 ya vifaa hivyo wanatengeneza wao.
(4)Iran ndo muuzaji mkubwa wa pikipiki kwenye mataifa ya Oman,Syiria,Iraq, Afghanistan, na Pakistan.
(5)Iran ni miongoni mwa mataifa machache duniani yanayo tengeneza mitambo ya uchimbaji wa gesi yenye teknolojia ya hali ya juu sana, hata sasa hivi Urusi ana tegemea mitambo ya Iran ili kuchimba gesi yake baada ya vikwazo vya mataifa ya Magharibi maana hapo awali alikuwa anatumia mitambo kutoka ujerumani.
(6) Iran ni mtengenezaji mkubwa wa mazuria ya kuvutia duniani.
(7) Iran inazalisha umeme zaidi ya Megawat 125,000 umeme ambao ni zaidi ya umeme unao tumika bara zima la Africa wakati Tz Megawat1600 tu.
(8) kwenye silaha sina haja ya maelezo mengi sana ana tengeneza vifaru,drone,meli,makombora ,satalaiti,nyambizi,mfumo ya ulinzi nk.
Hapo nimekuwekea machache tu kuhusu Iran sasa niambie utajilinganisha na taifa hili kwa lipi hasa?
Kuhusu raia wa Iran kwenda Ulaya ni kawaida ya binadamu kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine kutafuta furusa ,na ni haki kwa kila binadamu kwa mujibu wa sheria za kimataifa la msingi afuate taratibu.
Hata uko Ulaya na Marekani kuna baadhi ya raia wao wako kwenye nchi zingine tena masikini ukiwemo TZ wakitafuta furusa.