Kutambulishwa ukweni na kutolewa mahari sio uhakika wa ndoa

Kutambulishwa ukweni na kutolewa mahari sio uhakika wa ndoa

Mpesa, Tigopesa,Airtel money, Halopesa mnashindwaje Sasa kurudisha? Au wamesamehe na nyinyi mnalazimisha kuwarudishia?

Pole Sana mkuu heri uchumba uliovunjika, kuliko ndoa ya mateso
 
Nimewahi mimi binafsi,, nilitoa mahari, na kumvalisha pete baada ya miezi mitatu alinipigia kwa jeuri na kunitusi kisa nimepeleka mbele tarehe ya harusi hapo ndipo ukawa mwisho wa uchumba wetu, mama yake alichanganyikiwa alitaka wamuombee msamaha ila mimi sikuhitaji suluhu nae tena.
Dah we kwel ndume maan wangekua wengine ni full kujiliza-liza tu vip mahari walikurudishia au?
 
Kwa nini uliachawa na mahari ikasusiwa kabisa?
Yes imenitokea mimi binafsi nilitolewa mahari mwaka juzi na pete nikavalishwa. Haikuwa riziki miezi 8 baadae tukaachana na kila mtu akashika hamsini zake. Upande wa kiume hawataki kuchukua mahari zao ingawa tunafanya jitihada sana wazichukue. Kweli kabisa mahari sio ndoa wakuu.
 
Kwetu sisi watunza asili..na hata kibiblia..ukishatolewa mahali tayari wewe ni mke na mume wa mtu..hizo zingine ni mbwembwe tu za binadamu..ndio mana siku ya mahari ndugu wa pande mbili hujumuika pamoja.

Wenye dini za kuletewa komaeni na makanisa na misikiti...ila mwafrika halisi ukishalipia mahali wewe anza kuzaa ni mkeo halali huyo.

Wajinga na wafia dini hawata elewa si washangai ndio ujinga wao.

#MaendeleoHayanaChama

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Yes imenitokea mimi binafsi nilitolewa mahari mwaka juzi na pete nikavalishwa. Haikuwa riziki miezi 8 baadae tukaachana na kila mtu akashika hamsini zake. Upande wa kiume hawataki kuchukua mahari zao ingawa tunafanya jitihada sana wazichukue. Kweli kabisa mahari sio ndoa wakuu.
Dah!...
 
Kwa nini uliachawa na mahari ikasusiwa kabisa?
Sikuachwa mkuu tena hakuna sababu ya maana. Mama mkwe alikuwa anataka niende nae Moshi baada ya kusikia ninaenda kusalimia kwetu maandalizi ya kwenda kwetu yalikuwa tayari kabisa. Nikasema naomba niende nyumban kwanza nikirudi twemde moshi wakasema ( mama na mwanae) kama unaenda kwenu nenda moja kwa moja nikaondoka bila kugeuka nyuma.
 
Mimi nilipeleka barua ya posa sehemu kwa nia ya kutaka kuoa binti mmoja hivi, ila sikurudi tena baada ya binti kunitajia mahari kubwa tofauti na uwezo wangu na kuniwekea masharti ya kipumbavu.
Hata mshenga wangu niliyemtuma alishangaa hivyo hatukurudi tena.
 
Acha ni washe kengere ya Taarifa niendelee kusoma shuhuda maana mwenyewe naziona dalili za kumpiga chini mtoto wa watu kama hatabadilika..!
[emoji41][emoji41]
 
Mimi nmeshuhudia kabsa... classmate wangu (ke) alileta kadi ya mchango wa harusi home kwa ajili ya hafra ya ndoa, lakin siku chache mbeleni bwanaharusi mtarajiwa alipenyezewa habari kuwa mkewe mtarajiwa kuna mtu anammega....

Bwana harusi akapatiwa adi ushahidi wa pic,jamaa alisamehe kila kitu...wazazi wa bint walipata aibu sanaa.

Ila sema kuna mabint wanabahati zao...baada ya miezi kadhaa akatokea mwamba juzi tu ndo tumepiga mpunga wa ndoa.
Kuna watu wambeya kazi yao huwa kuharibia wenzao mahusiano utafikiri wao ni malaika, Bora dada aliolewa na huyo mwingine, kisicho ridhiki hakiliki
 
Yes imenitokea mimi binafsi nilitolewa mahari mwaka juzi na pete nikavalishwa. Haikuwa riziki miezi 8 baadae tukaachana na kila mtu akashika hamsini zake. Upande wa kiume hawataki kuchukua mahari zao ingawa tunafanya jitihada sana wazichukue. Kweli kabisa mahari sio ndoa wakuu.
Why mliachana, napenda mila ya kabila letu siku unatoa mahari ndio unavisha pete na ndoa inakuwa mwezi huo huo hamna kuchelewesha
 
Why mliachana, napenda mila ya kabila letu siku unatoa mahari ndio unavisha pete na ndoa inakuwa mwezi huo huo hamna kuchelewesha
Hamna Mambo ya vikao vya miezi mitatu..!!safi sana
 
Back
Top Bottom