Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Tuwe na akiba ya maneno jamani sio vizuri ulichoandika mkuu be humble 💔💔
 
Pole kwa msiba huu lulu diva,, nimpongeze kwa moyo wa kumuuguza mama yake hilo tu ni fundisho,kuhusu kujenga asingejenfa kwenye familia isiyomuhusu ktk kurithi hapo ni ujombani kwao,, na hata ingekuwa ni kwa baba zake wakubwa bado sio jukumu lake kupajenga,,

Ila humu wengi akili hazimo Yani, umaskini wa akili una gharama sana
 
Pole kwa msiba huu lulu diva,, nimpongeze kwa moyo wa kumuuguza mama yake hilo tu ni fundisho,kuhusu kujenga asingejenfa kwenye familia isiyomuhusu ktk kurithi hapo ni ujombani kwao,, na hata ingekuwa ni kwa baba zake wakubwa bado sio jukumu lake kupajenga,,

Ila humu wengi akili hazimo Yani, umaskini wa akili una gharama sana
Ukiachilia mbali UKIMWI na UTI ugonjwa mwingine unaotutesa watanzania ni wivu na chuki
 
Hiyo hela anayo sasa mkuu...uuguze na bado upige plasta ili watu sijui wasikucheke[emoji848]kumbuka yy ndo first n last born hana wa kumsaidia!

Daaah kama mambo yenyewe ndo haya nawashukuru sana kaka zangu kujenga nyumba mpya kijijini kuzaliwa wa mwisho raha asee[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Sina hakika mleta mada umri wake ukoje, uzoefu wake wa maisha ukoje hadi kuja na mada iliyojaa utoto mwingi kiasi hiki (with due respect).

Huyu dada nilimsikia mara moja muda mrefu kidogo—sikumbuki ni wapi—kuwa ana muuguza mama yake. Kwa aliyewahi kuuguza anajua ni kiasi gani lile jambo linaathiri pakubwa kisaikolojia, kikazi na haya kiuchumi—kuuguza kuna firisi. Lakini, pia uwezo wa mtu kifedha haupimwi kwa jina lake, pengine hilo jina na hizo mbwembwe ndio zilimfanya apate hata hicho kidogo alichotumia kumuuguza mama. Na pia, suala la kujenga nyumbani nalo si rahisi kama wengi wanavyolieleza hapa. Licha tu ya uwezo wa kifedha, wakati mwingine huwa kuna mivutano mikubwa ya kifamilia juu ya nyumba, kiasi cha kutia ugumu juu ya kuijenga nyumba hiyo. Lakini all in all, kwanini tumlaumu yeye Lulu Diva kwa kutokujenga kwao, badala ya kwanza kuwalaumu wazazi wake—ikiwa kweli watu tunaona kulaumu ndio njia sahihi? Yaani mimi nisijenge kwangu, kisha lawama zije kwa wanangu? [emoji848]
 
Mastaa wetu sijui wanakwama wapi mjini fujo kibao halafu home miyeyusho
Kupitia kanumba
Agnes masogange
Albert mangwea.

Inaonyesha jinsi gani wasanii wetu wanavyotudanga kwenye mitandao ya ukiwakumbusha unaambulia matusi,

Kuna lile uwoya ndo halijielewi kabisa kila siku lipo hotelini.
Masogange alijenga mbona kajumba kazuri kwa baba ake! Kushinda wote hapooo!!!
 
Nasema nyumba ya tope kwa sababu dar hajajenga anaongoza kwa kupanga mitaani huko hivo basi kwa kuwa yeye ni mtoto pekee wa mama na mama alikuwa na nyumba ya tope basi luludiva ndio anaweka record ya kurithi na kuishi nyumba ya tope

View attachment 2052860

View attachment 2052861
Imerekebishwa na mbabe mmoja mjini. Kaona aibu wanavyokula bata sana. Kayafanya haya ndani ya siku 2 au tatu muache ngebe
EC395229-8E68-4884-A08D-338D769695FB.png
 
Mimi nina miliki nyumba nzuri zaidi ya tano na mzazi wangu nimemrekebishia nyumba yake hapa Dar anaishi pazuri. Sisi kwetu kabisa ambapo tutazikwa ni Mtwara na huko sijajenga hata banda la bata.

Ina maana siku nikifa nikipelekwa huko ndio kutakuwa kwangu? Najenga nyumba zitakazoniletea faida nikipangisha, siwezi kujenga wakakae mijusi na mapanya. Kule nitaenda kuzikwa tu. Watotocwangu hawawezi kwenda kuishi Masasi huko kusiko na fursa
Mtwara ndo makaburini?!!
 
Mimi hapa namtetea, kamuuguza mamaake more than 5 years. Kamchukua mamaake akaenda kukaa nae mjini. Hakumuacha huko kijijini. Kuuguza kuna garama mno, specially yeye mamaake ali paralyze kwa muda mrefu. Mwenyewe alishawahi kusema. Operesheni ilim cost zaidi ya milioni 20 hapo kuna dawa ambazo ni garama. Mimi namuuguza mama naelewa.kuna pampers kwa siku unatumia 4.nazo ni garama.chakula chake tofauti.mtu wa kumchua, kufanyishwa mazoezi vyote sio bure. Kwa hiyo unaona priority mzazi wako hayo ya ujenzi huko vijijini huyapi kipao mbele. Na yeye amezaliwa peke yake mzigo mkubwa unakuwa wa kwako
 
Huwenda hapo ni kwa Babu yake, sio vizuri kumjaji mtu bila kuwa na taarifa kamili.
 
Mtu anauguza hizo nguvu za kujenga anazitoa wapi??? Muacheni Dada Lulu
 
Wengine wamemtete wakisema eti hapa duniani tunapita hakuna haja ya kujenga

Wengine wakasema amjengee nani wakati alikuwa na mama yake tu?

Kwetu tunasema ujenge nyumba ya kulinda makaburi.

Wengine wakamtete eti yeye akifa atazikwa kwa mme wake,je kama hotooelewa? Au akifa kabla ya hiyo ndoa? Ya mungu mengi simsemi vibaya.

Hatumsemi vibaya ila msanii anaeweza vimba mjini na gari kali atawezaje shindwa hata mili 10 tu ajenge nyumba ya kawaida?

Kama angekuwa sisi watu wa kawaida tusokuwa na mishahara sawa hakuna shida.

Wasanii wanamiliki simu za mil 3 anapanga nyumba ya laki 5 kwa mwezi iweje usahau kuna maisha ya baadae?
Mimi uwa mawachekesha watu ofisini.nawambia mimi kama akitokea mzamini akanininulia macho matatu naiuza nanunua sumsung ya laki 4 wanacheka.

Ni kwakuwa sina hela labda ndo maana nina uchungu na hela.

Kwakweli katia aibu. Na mimi nikifa leo mkaenda nizika home mtacheka kidogo sana kuwa nyumba yetu imepitwa na wakati ila sio tope .na pale nyumbani pembeni msingi nilouweka pale mwezi ulotipa sio wa kitoto mtajua ninakoelekea.

Mi siwezi chezea pesa, hata ikitokea fala moja akanihonga hata laki siku zote elfu 50000 lazima niitume nyumbani, cement kwetu ni 26000, nondo 27000 trip ya mawe 70000, mchanga 60000,boma linataka tofali 20000, nataka msauzi bati 70 leo nianze kutumia macho matatu? Ni upuuzi.
Ningekuwa na nafasi ya kama hawa wasanii ningefanya vitu vya maana sana

Wasanii ni watu wa ovyo kabisa.
Umeongea kwa uchungu sana.
Hapa pia wengi tunajifunza sana ili tusiyarudie makosa ya mwenzetu labda pia kupitia hili naye atajifunza pia.
Yawezekana pia kuuguza kumechangia yeye kuwa katika hali aliyonayo wenye kuuguza wataelewa.
Mimi nampa pole na Mungu amtie nguvu Mana ndie ndugu wa karibu na nguzo yake kaipoteza maumivu aliyonayo ni makubwa sana.
Tunajifunza kupitia changamoto za watu wengine.
Kumlaumu huyu bidada ni kumuongezea uchungu mana kazi ya kuuguza si mchezo hasa kama unapambana peke yako na hata kama unapata msaada inafika sehemu watu wanakuachia mzigo wako
 
Hapo ni kwa wajomba zake,ila kwa ugonjwa wa mama yake angejiandaa hata kwa kupiga hiyo nyumba plasta na sakafu ya block...lolote hutokea unapokua na mgonjwa ambae hawezi kupona
Shida ni kuwa ukiwaza ufanye ukarabati wakati mgonjwa bado anahitaji huduma na pesa zetu hizi za kuunga unga ndio unajikuta unaamua kukomaa tu na mgonjwa.
Hayo wanayaweza wenye pesa mana anaweza kufiwa ndani ya wiki nyumba ikajengwa ili sisi kina apeche alolo mtihani kwakweli.
 
Back
Top Bottom