Unajenga kwenu haujengi Nyumba ya Ukoo wewe peke yako!!!
Unaweza kuwa unawajengea wazazi wako, ila sio kuwajengea wajomba zako tena ambao wapo 9 ila wameshindwa kutumia akili.
Maisha yametofautiana ikiwa wewe unapambana kujenga kwenu, Lulu diva alikua anapambana kumuuguza mama yake!!
Kama ambavyo wewe unajenga kwenu kuna watu wazazi wao walishajenga makwao muda tu na wewe hapa wanakushangaa wazazi wako walishindwa vipi kujenga mpaka uje uwajengee wewe!!! maisha yametofautiana tusichekane tusibezane .....vipato na changamoto zipo tofauti.
binti mdogo asie na baba wala ndugu, kuuguza ugonjwa aina ule kwa miaka karibia 5 leo hii mnamsema kisa kujenga muwe na utu!!!