Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Tuwe na akiba ya maneno jamani sio vizuri ulichoandika mkuu be humble πŸ’”πŸ’”
 
Pole kwa msiba huu lulu diva,, nimpongeze kwa moyo wa kumuuguza mama yake hilo tu ni fundisho,kuhusu kujenga asingejenfa kwenye familia isiyomuhusu ktk kurithi hapo ni ujombani kwao,, na hata ingekuwa ni kwa baba zake wakubwa bado sio jukumu lake kupajenga,,

Ila humu wengi akili hazimo Yani, umaskini wa akili una gharama sana
 
Ukiachilia mbali UKIMWI na UTI ugonjwa mwingine unaotutesa watanzania ni wivu na chuki
 
Sina hakika mleta mada umri wake ukoje, uzoefu wake wa maisha ukoje hadi kuja na mada iliyojaa utoto mwingi kiasi hiki (with due respect).

Huyu dada nilimsikia mara moja muda mrefu kidogoβ€”sikumbuki ni wapiβ€”kuwa ana muuguza mama yake. Kwa aliyewahi kuuguza anajua ni kiasi gani lile jambo linaathiri pakubwa kisaikolojia, kikazi na haya kiuchumiβ€”kuuguza kuna firisi. Lakini, pia uwezo wa mtu kifedha haupimwi kwa jina lake, pengine hilo jina na hizo mbwembwe ndio zilimfanya apate hata hicho kidogo alichotumia kumuuguza mama. Na pia, suala la kujenga nyumbani nalo si rahisi kama wengi wanavyolieleza hapa. Licha tu ya uwezo wa kifedha, wakati mwingine huwa kuna mivutano mikubwa ya kifamilia juu ya nyumba, kiasi cha kutia ugumu juu ya kuijenga nyumba hiyo. Lakini all in all, kwanini tumlaumu yeye Lulu Diva kwa kutokujenga kwao, badala ya kwanza kuwalaumu wazazi wakeβ€”ikiwa kweli watu tunaona kulaumu ndio njia sahihi? Yaani mimi nisijenge kwangu, kisha lawama zije kwa wanangu? [emoji848]
 
Masogange alijenga mbona kajumba kazuri kwa baba ake! Kushinda wote hapooo!!!
 
Imerekebishwa na mbabe mmoja mjini. Kaona aibu wanavyokula bata sana. Kayafanya haya ndani ya siku 2 au tatu muache ngebe
 
Mtwara ndo makaburini?!!
 
Mimi hapa namtetea, kamuuguza mamaake more than 5 years. Kamchukua mamaake akaenda kukaa nae mjini. Hakumuacha huko kijijini. Kuuguza kuna garama mno, specially yeye mamaake ali paralyze kwa muda mrefu. Mwenyewe alishawahi kusema. Operesheni ilim cost zaidi ya milioni 20 hapo kuna dawa ambazo ni garama. Mimi namuuguza mama naelewa.kuna pampers kwa siku unatumia 4.nazo ni garama.chakula chake tofauti.mtu wa kumchua, kufanyishwa mazoezi vyote sio bure. Kwa hiyo unaona priority mzazi wako hayo ya ujenzi huko vijijini huyapi kipao mbele. Na yeye amezaliwa peke yake mzigo mkubwa unakuwa wa kwako
 
Huwenda hapo ni kwa Babu yake, sio vizuri kumjaji mtu bila kuwa na taarifa kamili.
 
Mtu anauguza hizo nguvu za kujenga anazitoa wapi??? Muacheni Dada Lulu
 
Umeongea kwa uchungu sana.
Hapa pia wengi tunajifunza sana ili tusiyarudie makosa ya mwenzetu labda pia kupitia hili naye atajifunza pia.
Yawezekana pia kuuguza kumechangia yeye kuwa katika hali aliyonayo wenye kuuguza wataelewa.
Mimi nampa pole na Mungu amtie nguvu Mana ndie ndugu wa karibu na nguzo yake kaipoteza maumivu aliyonayo ni makubwa sana.
Tunajifunza kupitia changamoto za watu wengine.
Kumlaumu huyu bidada ni kumuongezea uchungu mana kazi ya kuuguza si mchezo hasa kama unapambana peke yako na hata kama unapata msaada inafika sehemu watu wanakuachia mzigo wako
 
Hapo ni kwa wajomba zake,ila kwa ugonjwa wa mama yake angejiandaa hata kwa kupiga hiyo nyumba plasta na sakafu ya block...lolote hutokea unapokua na mgonjwa ambae hawezi kupona
Shida ni kuwa ukiwaza ufanye ukarabati wakati mgonjwa bado anahitaji huduma na pesa zetu hizi za kuunga unga ndio unajikuta unaamua kukomaa tu na mgonjwa.
Hayo wanayaweza wenye pesa mana anaweza kufiwa ndani ya wiki nyumba ikajengwa ili sisi kina apeche alolo mtihani kwakweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…