Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Maisha ya mitandaoni (kuigiza) si mazuri hata kidogo, pole kwake kwa kufiwa na mama yake kipenzi….
 
Kuwa na mchepuko mwenye mawazo kama yako ni kujiingiza katika mdomo wa mamba! Heri uchepuke la lulu diva maana k ni k tu
 
Sa afadhali hata yeye ana kwao, tena na Nyumba ya Tope ipo.. kuna wengine Tunamponda huku tumezaliwa kwenye Nyumba za Upangaji na mpaka leo tuko Kwenye Nyumba za Upangaji.. infact hatuna kwetu!!
Umeongea fact sana mkuu
 
Nachukia sana misiba kwa hili
Mimi nina Anko wangu mmoja alikuwa na cheo kikubwa tu cha polisi, ingawa ni kweli alikuwa ni mpenda bata lakini yeye alizaliwa Dar na mpaka amekuwa na kuwa mkubwa akijua kwao ni Dar na ndiko baba yake alijenga.

Alivyoingia kazini akaandika kwao ni Dar.

Sasa baba yake alifariki kwanza, ikabidi asafirishwe kwenda Musoma ( huko baba yake alikuwa na eneo kubwa tu ila ni kama alikuwa kawaachia ndugu zake tu ).

Baada ya msiba kuisha sasa ndio ikabidi jamaa aanze route za kwenda Musoma mara kwa mara na kutafuta njia ya kujenga hata kijumba.

Mara ghafla, mwaka juzi amedandia Noah akapata ajali wakafa watatu na yeye akiwemo.

Polisi wakaangalia documents zake, kaandika kwao ni Dar. Na huku Dar baba na mama hawapo, walishatangulia. Huku wamebaki wadogo zake ambao nao ni wahuni tu na kibaya zaidi vyumba vyite wamepangisha maana yake hata ysehemu ya kufikia wageni hakuna.

Kilichofuata polisi wakasema ukoo uamue, msiba upelekwe wapi kama ni Dar au Musoma. Ikabidi iwe Musoma.

Basi akapelekwa Musoma, lakini hakukuwa na nyumba ya maana. Nyumba iliyokiwepo ilikuwa ya mama mdodo na yeye anakomaa tu kibishi kujenga akiuza mahindi.

Hivyo ikabidi msiba ufukie humo.

Askari wenzake na ndugu baada ya musiba wakawa wanacheka na kupiga majungu balaa kwamba jamaa hata kujenga home ameshindwa.

Unaweza kuona mtu hajajenga home kumbe hujui yaliyoko nyuma ya pazia.
 
Shida hawa wanaojifanya ni maalufu hapa mjini wanaishi maisha ambayo mda mwingine ni mateso kwao mtu anahitaji kuishi KWA ghalama kubwa Ili aonekane ni matawi ya juu kumbe ni choka mbaya tu
na hii inawatesa sana
siku zote epuka kuishi maisha ya kuigiza yatakutesa siku moja
 
Ukweli ni kuwa watu wengi wanapoteza mda DSM Kwa maisha ya kuigiza.....!! Watu wanavimba Instagram, Wanaigiza Wana maisha mazur , nyumba, gari kumbe ni kulanda landa tuuu mjini , Kwa jina la Lulu Diva lilivyo mtaani ni ngumu kuamini kama alishindwa kumjengea mama yake hata mgongo wa tembo ya vyumba viwili...!! Kama huna mchongo wa kueleweka mjini Bora urudi stimbi ukajipange upya
 
sis watanzania tunaakil ndogo sana kwaio unahis waltoka kijijin na kuja kupanga mjin? kama taratbu za kwao n kuzka maeneo ya nyumban kwao ndio wajengee ukoo mzma nenda uchagan uone wachaga wananyumba za kawaida lakn uko mjin wana ma hekalu
Wachagga hawana nyumba za tope acha kudaganya kule nyumba nyingi ni nzuri kuliko hata za huku Dar kwenye msongamamo na uchafu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…