Mimi nina Anko wangu mmoja alikuwa na cheo kikubwa tu cha polisi, ingawa ni kweli alikuwa ni mpenda bata lakini yeye alizaliwa Dar na mpaka amekuwa na kuwa mkubwa akijua kwao ni Dar na ndiko baba yake alijenga.
Alivyoingia kazini akaandika kwao ni Dar.
Sasa baba yake alifariki kwanza, ikabidi asafirishwe kwenda Musoma ( huko baba yake alikuwa na eneo kubwa tu ila ni kama alikuwa kawaachia ndugu zake tu ).
Baada ya msiba kuisha sasa ndio ikabidi jamaa aanze route za kwenda Musoma mara kwa mara na kutafuta njia ya kujenga hata kijumba.
Mara ghafla, mwaka juzi amedandia Noah akapata ajali wakafa watatu na yeye akiwemo.
Polisi wakaangalia documents zake, kaandika kwao ni Dar. Na huku Dar baba na mama hawapo, walishatangulia. Huku wamebaki wadogo zake ambao nao ni wahuni tu na kibaya zaidi vyumba vyite wamepangisha maana yake hata ysehemu ya kufikia wageni hakuna.
Kilichofuata polisi wakasema ukoo uamue, msiba upelekwe wapi kama ni Dar au Musoma. Ikabidi iwe Musoma.
Basi akapelekwa Musoma, lakini hakukuwa na nyumba ya maana. Nyumba iliyokiwepo ilikuwa ya mama mdodo na yeye anakomaa tu kibishi kujenga akiuza mahindi.
Hivyo ikabidi msiba ufukie humo.
Askari wenzake na ndugu baada ya musiba wakawa wanacheka na kupiga majungu balaa kwamba jamaa hata kujenga home ameshindwa.
Unaweza kuona mtu hajajenga home kumbe hujui yaliyoko nyuma ya pazia.