Wengine wamemtete wakisema eti hapa duniani tunapita hakuna haja ya kujenga
Wengine wakasema amjengee nani wakati alikuwa na mama yake tu?
Kwetu tunasema ujenge nyumba ya kulinda makaburi.
Wengine wakamtete eti yeye akifa atazikwa kwa mme wake,je kama hotooelewa? Au akifa kabla ya hiyo ndoa? Ya mungu mengi simsemi vibaya.
Hatumsemi vibaya ila msanii anaeweza vimba mjini na gari kali atawezaje shindwa hata mili 10 tu ajenge nyumba ya kawaida?
Kama angekuwa sisi watu wa kawaida tusokuwa na mishahara sawa hakuna shida.
Wasanii wanamiliki simu za mil 3 anapanga nyumba ya laki 5 kwa mwezi iweje usahau kuna maisha ya baadae?
Mimi uwa mawachekesha watu ofisini.nawambia mimi kama akitokea mzamini akanininulia macho matatu naiuza nanunua sumsung ya laki 4 wanacheka.
Ni kwakuwa sina hela labda ndo maana nina uchungu na hela.
Kwakweli katia aibu. Na mimi nikifa leo mkaenda nizika home mtacheka kidogo sana kuwa nyumba yetu imepitwa na wakati ila sio tope .na pale nyumbani pembeni msingi nilouweka pale mwezi ulotipa sio wa kitoto mtajua ninakoelekea.
Mi siwezi chezea pesa, hata ikitokea fala moja akanihonga hata laki siku zote elfu 50000 lazima niitume nyumbani, cement kwetu ni 26000, nondo 27000 trip ya mawe 70000, mchanga 60000,boma linataka tofali 20000, nataka msauzi bati 70 leo nianze kutumia macho matatu? Ni upuuzi.
Ningekuwa na nafasi ya kama hawa wasanii ningefanya vitu vya maana sana
Wasanii ni watu wa ovyo kabisa.