Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Sio kweli ,wachaga nyumbani kwao migombani kuna MANSIONS ambazo wanazitumia wakati wa Xmas wakiwa mapumzikoni lakini muda mwingine wote zinakuwa nyumba za panya!!!
The problem mnachanganya kati ya Wachaga na Wachaga Wenye Uwezo kiasi kwamba mnataka kuaminisha watu Wachaga wengi wana mansions wakati uhalisia ni Wachaga wachache mno wenye hizo unazoita mansions na majority wana nyumba za kawaida tu, na wengine hata hizo za kawaida, hawana!! Kikubwa ninachokiona na kunifurahisha kwa Wachaga ni kile ambacho siku hizi kinaanza kuenea kwenye vijiji vingine. Uchagani, tangu zamani hizo, walikuwa wanajitahidi sana kujenga nyumba za bati hata kama ni ndogo wakati vijiji vya maeneo mingine zikijaa nyumba za tope na majani.
 
Best nikuambie kitu ukiamua hushindwi,ila tunajifunza kupitia matatizo yetu
 
Kushangaa ni kuishi nyumba ya tope huku mjini akivimba na gari ya milion 30
UIna mawazo ya kizamani sana! Yale mawazo ya"unaanzaje kununua gari wakati unaishi nyumba ya kupanga"! Mawazo ya ujima yanayodhani gari kwa mahali kama Dar ni anasa!!
 
Kwa sie tuliotoka kuuguza juzi juzi tu huku tukiwa hatuna kampani, tutakuelewa sana!! Watu ambao katu sitajaribu kuwa-judge ni mtu anayeuguza au mwenye watoto na/au tegemezi wanaosoma private schools!
 

unavoeleza inaonyesha kisaikolojia haupo sawa !.kuna kitu kina kusumbua kwenye hili swala kuhusu kwenu na angalau hata katofali kwenu
 
Hayo ni makaburi ya ukoo na hiyo ni nyumba ya ukoo wala sio kwake Luludiva.

Huyo dada ni mpambanaji na ametokea familia ya chini sana na ananyanyuka na amefikia hatua kubwa tu mpk ya kumiliki magari na kupanga nyumba nzuri. Na kwa sasa anajenga nyumba nzuri tu Ila bado haijaisha.

Ni wangapi humu wenye elimu mara 5 ya Lulu Diva na wanakwea daladala na hawajui lini watamiliki hata bodaboda? Ni wangapi humu wanashindwa hata kulipa kodi ya chumba kimoja? Ni wangapi humu hawana hata kiwanja a hili mbali msingi wa nyumba?

Tusimhukumu kwa kuangalia nyumba ya kwenye eneo la ukoo.
 
Mimi nina miliki nyumba nzuri zaidi ya tano na mzazi wangu nimemrekebishia nyumba yake hapa Dar anaishi pazuri. Sisi kwetu kabisa ambapo tutazikwa ni Mtwara na huko sijajenga hata banda la bata.

Ina maana siku nikifa nikipelekwa huko ndio kutakuwa kwangu? Najenga nyumba zitakazoniletea faida nikipangisha, siwezi kujenga wakakae mijusi na mapanya. Kule nitaenda kuzikwa tu. Watotocwangu hawawezi kwenda kuishi Masasi huko kusiko na fursa
 
Kila kitu kinaenda kwa mipango...Sasa ulitaka ajenge hapo halafu akae Nani??

Pia kuna vijiji ukijenga nyumba nzuri wanakijiji wanakuonea wivu kinachofata ni kurogwa
Usharogwa mara ngapi?
Unaushirikina sana weye unaonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…