Kutana na Luludiva; superstar anayeishi nyumba ya tope

Zikwa dar sasa usiende mtwara
 
JAMANI MTU KAUGUZA MAMA YAKE MIAKA 9 UGONJWA USIOPONA
UNATEGEMEA ANGEJENGA VIPI?
ACHANE UNAFIKI BWANA
Gari ananunua vipi?
Acha kutetea kwanza unajua kisa cha mama ake kuumwa vile?
 
Tusipende sana kukosoa kila kitu jamani, dada wa watu kapambana mno kumuuguza mama yake tena kwa muda mrefu, na kuuguza kulivyo gharama sasa..
 
Gari ananunua vipi?
Acha kutetea kwanza unajua kisa cha mama ake kuumwa vile?
Wewe kama una bifu binafsi na huyo binti mfuate. Lakini acha kuleta story za kunanga watu tena watoto wa kike waliojitoa kupambana kutafuta maisha kwa njia yoyote. Shida yako ni gari la Luludiva badala ya nyumba? Hayo ni maamuzi yake, wewe kama unaona nyumba ni muhimu kuliko usafiri ni maamuzi yako hatukukosoi.
 
Una akili Sana Dada mungu akutie wepesi na ufanikishe hitaji lako kwa hii attitude yako tu wewe ni Shujaa, Mimi nna ndugu zangu wengi wanapambana kuboresha na kujenga majumba yao tu, wanasahau kuwa hata wazazi wao wanahitaji maisha mazuri, Nipo napambana kuhakikisha wazazi wangu wanaishi vizuri
 
Kwanza vya nini vyote hivyo si unaona kadanja kaacha kila kitu[emoji848]
Kusema za ukweli lazima mtu uandae pahala pa kuzikwa. Kama hujajenga bora kueleza ndugu na Jamaica kuwa nikifa zikeni kinondoni full stop. Wewe umeenda lakini aibu unaachia walio hai. By the way nyumba yangu ya kwanza nilijenga kijijini. Usisahau kuna kufiwa na huwezi kukataza au ukachagua watu wa kuhani. Aidha ndugu zangu wa TA mbona mnaniangusha pamoja na mashauzi yenu? Nyumba za tope karne hii hapana
 
Pumba tupe ww umejenga kwenu ebu tuachege unafiki na uwongo

Maisha ya leo huwezi jenga kla sehemu unakaa dar ujenge na kijijini nako ujenge

Kwa kipato kipi cha wasanii ad aweze kujenga kijijini na mjini wapo mabilionea , na Viongozi kibao hawajajenga vijijini kwao acha uyo maskini mwenye jina kubwa
 
Lakini si kutumia k ili uwajengee wazazi
 
Kwani lazima uzike kwenu? Kinondoni hakupo? Usisahau kinondoni inakuepusha na hizi fedheha
 
Mtoe Ngwea na Kanumba hapo
 
Usanii ni GHARAMA sana. Ukiwa msanii kila jicho linakuangalia wewe, wengi wanakuangalia kwa jicho la kukuhukumu na kutafuta kosa na udhaifu wako, ikitokea umekosea kidogo tu, watu wataongea mazito mpaka yasiyokuwepo.

Wasanii wetu wanahisi maisha ya starehe tunayowaona nayo wanayoigiza kwenye runinga ndiyo wanayotakiwa kuishi mitaani, wanaishi maisha ya starehe kulinda hadhi ya umaarufu wao pasipo kukumbuka kujijenga kimaisha. Mwishowe siku zinapita pesa umechezea kwa starehe halafu hujafanya chochote cha maana.


Wasanii mkumbuke kujiimarisha kiuchumi mapema, na kukumbuka kwenu (kujenga nyumba ya kisasa kwenu).
 
Mimi sioni cha ajabu hapo. Lulu Diva ni mpambanaji tu kama walivyo watu wengi nchi hii.

Alianza kuigiza, mambo yakagoma, akawa video vixen na sasa hivi anakomaa na kuimba.

Sasa sioni popote kama kuna sababu ya kushangaa.
Watu wanashadadia tu ili kupata ahueni ya depression zao
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…