Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Bado naamini PSRS ni sehemu salama zaidi kwenye ajira, PSRS ifanyiwe maboresho makubwa kama kuajiri watumishi wengi wa kuwezesha michakato ya ajira kwa haraka na wepesi lakini hili la Taasisi kuajiri wenyewe malalamiko ni mengi sana na CCM ikifanya mzaha itachochea Chuki na hasira kwa vijana na inaweza kupelekea maamuzi ya hasira 2025.

Kilichofanywa na NSSF kitafanywa kwingine kama kisipodhibitiwa.

1. Mchakato wa ajira uwe wazi na huru kwenye taasisi za serikali hata kama taasisi zinaajiri zenyewe basi pasioneshe namna ya upendeleo wowote.

2. Kujitolea ni sawa lakini kisiwe kigezo Cha ajira maana huko mbeleni tutashuhudia makubwa kwenye kujitolea. Kama kitatumika kama kigezo, nafasi za kujitolea zitaadimika na kufanya zitolewe Kwa upendeleo.

3. Mpaka mtu kaamua kujitolea yanakuwa ni mapaenzi binafsi ya mtu hivyo isitumike kama njia ya kumuajiri moja kwa moja kama kumlipa hisani au fadhila anayefanya hivyo.

Tafadhali Rais Samia tazama hili suala kwa jicho la tatu, rejesha michakato ya ajira UTUMISHI
 
hizi ndio agenda vijana, tuzipiganie watawala wamekua wabinafsi sana
 
PSRS imesaidiq sana tena sio kitoto ,ndio maana sasa makazini kuna chuki watu walishazoea majina fulani daily , leo hakuna ule umbea kwa sababu za watu wa jamii moja.

Watu wapya daily mpaka raha sio kama zamani watu wale wale ,wakati wengine elimu wanazo ila hawapo kweny system.
 
HAPANA!! Huko NSSF kuna interns wengi sana walioingizwa huko kwa gia za kujitolea, na baadhi yao wakapewa hiyo mikataba mifupi mifupi. Zoezi zima lilianza pasipo uwazi na kwa upendeleo!! Sasa wanataka waingie "king"!! Ajira kwenye utumishi wa umma lazima ziwe wazi kwa watanzania wote bila kubagua!! Hapa panafuka moshi!!
 
Rais wetu naomba ulipe uzito jambo hili!! Kama tumefika pahala mtu anaamua tu kufanya ubaguzi na upendeleo wa wazi kiasi hiki kwenye ajira bila hofu yoyote!! Hii inatisha sana!! Vinginevyo wananchi watachukulia kuwa huu ubaguzi una baraka za mkuu wa nchi!!
 
Nafasi za ajira lazima ziwe wazi kwa watanzania wote weye sifa!! Siyo kinyongo bali ni kupigania haki!! Hao waliopewa hiyo mikataba kwanza haikuwa kwenye ushindani wa wazi!! Watu wamepachika ndugu zao hapo, hii haikubaliki!!
kwa hiyo uliytaka mm nikose upewe wewe. wacha zako mkuu pambana sehem nyingine
 
Wako sahihi Kwa sababu hakuna sababu ya msingi kwenda kuita watu wengine huko wakati Wana watu wa mikataba humo ndani.

Point ya msingi iwe kazi za mkataba ziwe zinatangazwa na watu wanaomba Ili zikipatikana za kudumu ndio wanapewa kipaombele.

Mwisho mashirika yameruhusiwa Kuajiri yenyewe
 
Laiti kama ingekuwa hao wanaofanya kazi kwa kujitolea waliingia kwenye hiyo taasisi kwa kufanyishwa interview isingelikuwa shida.

Tatizo linakuja kwamba wengi wao huwa wanaingia kufanya kazi za kujitolea kwa kuingizwa kindugu ama wengine kutoa rushwa ya ngono. Ukichunguza hapo asilimia 99% wameingia kindugu na wengi wao huwa wanakuwa shallow hatari katika utendaji kazi.

Kama wanataka kuajiri internal basi kuwepo pannel huru ya kufanyisha interview ambapo wataweka pass mark. Ikitokea imeshindikana kupatikana katika passmark zilizowekwa basi nafasi zitangazwe external. Vinginevyo hiyo taasisi wanataka kujazana ndugu na vimada wa watu tu.

Ila serikali inabidi iangalie sana kuhusu swala la ajira. Sasa hivi kumekuwa na rushwa sana kwenye ajira za serikalini. Yaani imefika mahali hadi nafasi za jeshini mtu anambwa atoe rushwa ya milioni mbili ili kuapatiwa nafasi. Watu wasiokuwa na connection ama fedha ya kutoa rushwa kupata kazi wamekuwa wanyonge sana kwenye hii nchi. Mbaya zaidi wanaohusika wapo kimya maana wanajua watoto na ndugu zao wana uhakika na kazi.

Eeh Mwenyezi Mungu tunakuomba uwajalie watu wako riziki wanazoporwa na watu waliojaa ubinafsi katika nchi yetu ya Tanzania.
 
kwa hiyo uliytaka mm nikose upewe wewe. wacha zako mkuu pambana sehem nyingine
Hakuna anayetaka wewe ukose, hakuna anayesema aliyejitoa au aliyekuwa na mkataba mfupi asiruhusiwe kuomba hizi nafasi za ajira. Wewe omba lakini lazima upambanishwe na waombaji wengine ambao hawakuwa na mkataba au hawakuwa wanajitolea!! Kama ukipenya basi upenye kupitia ushindani wa haki ulio wazi kwa watanzania wote!! Tunachokataa ni hii mbeleko ya aibu inayotaka kuwabeba na kuwakinga na ushindani ulio wazi kwa wote!
 
Nafasi za ajira lazima ziwe wazi kwa watanzania wote weye sifa!! Siyo kinyongo bali ni kupigania haki!! Hao waliopewa hiyo mikataba kwanza haikuwa kwenye ushindani wa wazi!! Watu wamepachika ndugu zao hapo, hii haikubaliki!!
Mnataka mtangaziwe kama geresha?? Na mwisho wa siku wao wachukue wale wa ndani pekee. Si mtaanza kulalama kuwa mmechoma nauli zenu??
 
Kwa Hali hii niambie uko kazini kuna kuwajibishina kwel madudu yakitokea, utendaji wa kazi utakuwaje kama sio ovyo ovyo Nani amuadhibu Nani, hii haikubaliki nini tunaenda kutengeneza uko makazini ni rushwa za kila Aina, ufisadi uliobobea, ukabila usipingika kila kitu kitakuwa ovyo ovyo, Raisi wetu mama Samia naomba uingilie Kati ili suala
 
Izo nafasi za kujitolea pia niconnection ndo maana tunapinga. Ingewezekana ata izo nafasi za kujitolea wazitangaze watu waombe sio kwa namna Mfumo ulivyo sasa
 
Hii haikubalikii inatia hasiraa saana ni bora tu CCM waseme tuu kwamba sisi watoto wa masikini hatuna hakii ya kuajiriwa serikalini,,wanatumia gia ya kujitolea wakatii nafasii ya kujitolea huwezii kuipataa kama huna connection,,ila Mungu yupo the freedom is coming soon,,, PSRS NDIO MTETEZI WETU
 
Hapa Magufuli alikuwa sahihi nakuambia kuna watu wapo taasisi nyeti wapya kabisa ila hato mwanzo hawakuwepo na baadae mtu anasema watu fulani hawana elimu Wakati walipata ubaguzi wa fursa tangu zamani ,wanasoma wanaishia kufanya biashara ila kazi serikalini hawapati.


Bro kuna msela aliomba inteership na alikuwa yupo vizuri akaambiwa hakuna tena mlango wa HR una tangazo kabisa "Hakuna nafasi za kujitolea wala mafunzo ya vitendo" ....wiki kadhaa wakaenda wengine tena wakapata wote wana ukaribu na HR ...

Yaliyopo ndani yanasikitisha kwe kweli.
 
 
Aliyesababisha haya yote ni mtu mmoja alipewa shirika aendesha akafanya kama vile ni la familia yake.
Alianza kuondoa wote waliotumikia kwa mda mrefu na kuleta wengine wengi zaidi ya 500 ambao alidhani angewamudu kuwa endesha atakavyo kwa mikataba mifupi.
Na hao waliopewa hyo mikataba walipewa kufanya kazi very sensitive.
Wengi wao ndo wameambiwa waombe kazi ili wapate permanent employment.
 
Mtendaji mkuu wa NSSF amevunja katiba ya nchi ibara ya 13, inayokataza ubaguzi wa aina yoyote. Kutangaza ajira kwa kuwabagua baadhi ya waombaji watanzania wenye sifa, huko ni kukiuka katiba ya nchi, AWAJIBIKE AU AWAJIBISHWE!!

Katiba nya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, ibara ya:
13(4). Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au na mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.

NSSF imekiuka klifungu hiki cha katiba ya nchi yetu kwa kuwabagua watanzania wengine wote wenye sifa za kuomba ajira zilizotangazwa pale NSSF, na kuwapendelea watanzania waliomo ndani ya NSSF aidha kwa kujitolea au kwa mikataba mifupi (ambao bila shaka waliingia humo kwa kupendelewa pia-uchunguzi inabidi ufanyike) ili wao pekee ndio waziombe nafasi hizo za ajira!

Inabidi Mtendaji mkuu wa NSSF ajiuzulu kwa kuvunja katiba ya nchi yetu! Hili jambo siyo dogo, na wakilipuuzia tutaenda mahakamani!! Maana haki, wajibu na maslahi ya kila mtu hulindwa na mahakama kwa mujibu wa ibara ya 13(3) ya katiba ya nchi nyetu inayosema: Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu na jumuiya ya watu yatalindwa na kuamuliwa na mahakama na vyombo vinginevyo vya mamlaka ya nchi vilivyowekwa na sheria au kwa mujibu wa sheria.
 
Serikali ya CCM ni afadhalii ikachezaa na vitu vyote ila sio kufanya mchezo na jobless,,NSSF wanatuletea takataka zao hizo eti ni tangazo la kazi bila hata AIBU,,,,Mkurugenzii wa NSSF atujibu kuwa ni lini walitangaza hizo nafasii za mikataba,,,UPUUZI huu haukubalikii hata kidg tutaukataa kwa nguvuu zotee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…