KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,789
- 4,951
Bado naamini PSRS ni sehemu salama zaidi kwenye ajira, PSRS ifanyiwe maboresho makubwa kama kuajiri watumishi wengi wa kuwezesha michakato ya ajira kwa haraka na wepesi lakini hili la Taasisi kuajiri wenyewe malalamiko ni mengi sana na CCM ikifanya mzaha itachochea Chuki na hasira kwa vijana na inaweza kupelekea maamuzi ya hasira 2025.
Kilichofanywa na NSSF kitafanywa kwingine kama kisipodhibitiwa.
1. Mchakato wa ajira uwe wazi na huru kwenye taasisi za serikali hata kama taasisi zinaajiri zenyewe basi pasioneshe namna ya upendeleo wowote.
2. Kujitolea ni sawa lakini kisiwe kigezo Cha ajira maana huko mbeleni tutashuhudia makubwa kwenye kujitolea. Kama kitatumika kama kigezo, nafasi za kujitolea zitaadimika na kufanya zitolewe Kwa upendeleo.
3. Mpaka mtu kaamua kujitolea yanakuwa ni mapaenzi binafsi ya mtu hivyo isitumike kama njia ya kumuajiri moja kwa moja kama kumlipa hisani au fadhila anayefanya hivyo.
Tafadhali Rais Samia tazama hili suala kwa jicho la tatu, rejesha michakato ya ajira UTUMISHI