Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Tafadhali mekeni na kwenye mitandao mingine yakijamii ili tukatag watu nakushare mpaka waone aibu hawaaa
 
Moto utawaka!! Mtu ataridhika akikosa kazi kwenye ushindani wa wazi, siyo kwa kubaguliwa namna hii mchana kweupe!
 
Huyo nae alikuta tatizo ambalo lilianzia Kwa Dr.Dau Kwa kutumia njia hiyo hiyo kuwabagua wagalatia,na kujaza jamaa wa Imani Kali wakageuza NSSF ni ya kwao
 
Watoe fair competition kwa wote wenye sifa.
Haiwezekani mtumishi ndani ya taasisi ajira yake education level ilikuwa diploma,then aka upgrade na kuwa bachelor holder. Halafu nafasi inapatikana ya mtu mwenye bachelor utegemee achukuliwe wa nje ya taasisi, hiyo never. Na ndio maana Kuna internal recruitment
 
Sasa kama that is the CASE, kwann wanaojitolea taasisi nyengine wasiruhusiwe kuomba ?? Wakati wote ni wanajitolea??? Yani kwann anayejitolea Halmashauri asiombe?? Wakati zikitoka za Halmashauri huyo wa NSSF Ataomba.
 
Kwa kawaida kwa nafasi zilizo nyingi mchakato wa usaili huwa na hatua mbili: 1. Usaili wa kuandika (written), 2. Usaili wa mahojiano (oral). Kwa sasa kwenye written nafasi moja hugombaniwa na watu wasiopungua 100 (kwa uchache). Kwa hiyo hizo nafasi 392 kwenye hatua ya written inabidi zigombaniwe na watu 39,200. Ina maana huko NSSF kuna watu wa mikataba na wa kujitolea zaidi ya 30,000? Kama sivyo, kwa nini warahisishiwe hivyo wakati kuna malaki ya watanzania wanaotafuta ajira? Kwa nini hawa wapendelewe kwa kuepushwa na ugumu wanaokabiliana nao waombaji wengine kupitia PSRS?

Hata kama huko NSSF wataamua kusiwe na written baliu ni oral tu, hata hivyo kwa sasa nafasi moja kwenye oral huwa inagombaniwa na waombaji wasiopungua 5, ina maana huko NSSF kuna wjitoleaji na watu wa mikataba zadi ya 1,900? Hiyo mikataba ilitangazwa wapi? hizo nafasi za kujitolea zilitangazwa wapi? Hii haikubaliki hata kidogo!! Ninachokiona ni baadhi ya "wateule" kupita bila kupingwa maana hakuna wapinzani!! Hii haikubaliki hata kidogo!!! Kuna mtu asiyejua kuwa kuna malaki ya wasaka ajira mitaani tena wenye sifa stahiki kabisa!!
 
Internal recruitment ni kwa wale wenye ajira tayari! Akijiendeleza ndani ya ajira na kupata degree kwa mfano, huyo anafanyiwa re-categorization!! Hakuna internal recruitment kwenye ajira mpya!! Patachimbika hadi mahakama ya rufaa ikibidi!! Wasipotrusikiliza, mchakato wa ajira utasimamishwa kwa COURT INJUCTION!! hadi pale kesi ya msingi ya tuhuma za kutaka kuajiri kwa misingi ya ubaguzi kinyume na katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 13(1&4), itakaposikilizwa na kufanyiwa maamuzi.
 
Huyo nae alikuta tatizo ambalo lilianzia Kwa Dr.Dau Kwa kutumia njia hiyo hiyo kuwabagua wagalatia,na kujaza jamaa wa Imani Kali wakageuza NSSF ni ya kwao
Naomba sana huko kwenye udini tusiingie, kutatuondolea mshikamano wetu.!! Hapa wamebaguliwa dini zote walio nje ya NSSF kwa sasa!! Wanataka kuifanya NSSF kama familia fulani ya wateule fulani!!
 
Hiyo nafasi ya kujitolea iko sawa kwa wote?
Wapi wanaotaka kujitolea na hawapati nafasi hizo.
 
Nenda ukajitolee baada miaka 3....utaajiriwa zikitoka tena
 
Uko sahihi sana.
 
Hapa tutaona kama serikali yetu ni sikivu kama ambavyo huwa inadai. Haiwezekani taasisi inayogharimiwa na kodi za watanzania wote, iamue kuwatenga na kuwabagua watanzania walio wengi kwenye ajira!!
Ila hili pendekezo mbona hata bungeni lilitolewa na Spika....mlipiga kelele? Huenda watu ndio wanafanyia kazi ushauri kifupi siki hiz kupata kazi ni kazi. Walianza na vigezo vya kupita JKT...watu wakawa wanapigwa chini...sa hii imeletwa gia mpya! KUJITOLEA. Tutanyoooka tuπŸ˜…πŸ˜…πŸ˜…
 
Tulipiga kelele ndiyo, na sasa wataona kuwa kumbe makelele yetu hayakuwa ya mchezo!! Huyo spika naye ni wa kumhurumia tu!! Yuko pale kutumiwa!!
 

Huyo jamaa anadhani wote humu tuna akili kama zake, inawezekana nae anasubiri kula pande huko NSSF kupitia tanngazo lao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…