Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Tena kwa kiburi tuone nini na Nani ni Nani, mkuu sijawahi kufikiria kama kunaeza tokea watu wa ajabu kiasi hiki, yaan wameamua Bora iwe Ivo Ivo...
Ni mambo ya ovyo , hata lile suala la vyeti feki na watumishi hewa ilikuwa ni moja ya sababu ya kuanzisha huu mfumo wa PSRS ili kudhibiti mianya ya watu wasio na sifa kuingia kwenye hizo taasisi kama ilivyokuwa inafanyika zamani .
Sasa kuna wapuuzi wanaharibu mfumo huu ili wapate mianya ya kupenyeza hata wasio na sifa .
Sasa mfumo wa kihuni unarudishwa ,that's means tunarudi kule kule kwenye Madudu ya kuuza nafasi za kazi kwa rushwa na nepotism haya kwa wasio na sifa na hata kutengeneza watumishi hewa
Ni nani ataensure credibility ya hao wanaoajiriwa ?
Halafu unakuta taahira mmoja anasupport ujinga kama huu .
Hii haikubaliki
Hii nchi inautaahira mwingi sana
 
mnatumia madhaifu yake kuonyesha ubaguzi wa wazi kabisa.....
Tunambagua ubaguzi wa nini, wa rangi ?

Umekiri kwamba ana madhaifu, tukikosoa madhaifu yake unasema tunabagua

Tunambagua kwa hali gani aliyo nayo, ulemavu, uweupe, umwanamke, umaskini, ukoma? Eleza Samia ana hali gani ya kinyonge au ya kipekee hapa Tanzania ya kufanya jamii imbague!
 
Shida hujui kama hata kujitolea nayo inahitaji connection ni vigumu kupata nafasi ya kujitolea sehemu bila connection labda kama hiyo sehemu hawakupi chochote ndo maana tunataka fair competition
Fairness is an illusion boss... Mtaongea bt nothn gonna change coz ajira za serikalini ni kwaajili ya watoto wa wakubwa tu na hizo little opportunity zinazojitokeza ndio wana cover watoto wa masikini so don't expect Fair Competition

Sent using Jamii Forums mobile app
 
unavyojua ww ubaguzi mpk wa rangi et....
Ila tabaka mwenye nacho na asikuwa nacho hamlioni et....
Hii nchi aliyesema mbinguni ni station ya vituko hajakosea....
 

Tasisi zote zinayo Human Resource Policies Manual.
Manual hii ndio msingi wa tangazo kama hili.
Kwa hiyo, unaweza kukosoa tangazo hili kwa kuanzia katika manual hiyo.
Vinginevyo unakuwa huna uhakika na unalolisema.
Utaonekana hujawahi kufanya kazi katika taasisi kubwa kama NSSF unayoitaja.
Utafiti mwema.
 
Halfu mleta mada uwe na uhakika na jambo ndiyo ulitolee maelekezo,unajua ya kuwa shirika linaongozwa na bodi so maamuzi mpaka kufikia hapo bodi imeyapitia kabla ya utekelezaji sioni upendeleo waliofanya NSSF naona wakitoa fursa kwa watanzania kwanza NSSF ni taasisi ya serikali iliyo kaa muda mrefu bila kuaajiri kwahiyo acha mfuko uajiri upate nguvu kazi ya kutosha usiponufaika wewe kwenye kupata ajira zao basi atakuja nufuaika hata mtoto wako, mjukuu wako,kitukuu wako,shangazi na mjomba wako so usione kama mfuko unabagua watanzania wanaopatiwa hao pia ni watanzania usiweke roho ya kinyonge, watanzania wengi wamekaa njee ya ajira za serikali kwa muda tangu uongozi wa magufuli sasa acha mifuko na taasisi zingine za serikali ziajiri
 
Kwa hiyo vijana waliopata kazi wafukuzwe, au vipi?
 
Badala ya kulalamika Serikali ilete Sera za kuongeza Ajira watu wapate ujira unalalamika na kungangania na mwendelezo wa kugawana kidogo (badala ya kuongeza hicho kidogo kiwe kingi)
 

Hii ni internal vacancy announcement, wewe inakuhusu nini? Au hujui kizungu, hivi unafikiri ukikimbilia court unapata unachotaka tu, acha wivu wa fisi
 
Hii inashangaza sana lakini huwezi kuwaingilia NDO wameshaamua,mawakili wanakazi zao hawawezi kuwasumbukia watu wengine wasio na maslai kwao ,kwani mawakili wakipata misukosuko na kukamatwa ,kupigwa na kumbambikiziwa kesi Mimi na wewe tunajificha ndanina kuangalia kwenye WhatsApp yanayo wapata,Kwa mfumo huu tutahangaika sana.
 
Kwanini wakati ajira zinapitia utumishi walikuwa hawaajiri? Sasa hivi wameruhusiwa kuajiri wenyewe wameibuka na nafasi 300+
Walikuwa wanaogopa nini kuzipeleka utumishi? Huoni kuwa vijana wao walikuwa wanafeli usaili?
 
Hiyo human resource policy ndio ilileta vyeti feki. Maana hapo watazoa tu ndugu zao. Mwalimu atapewa nafasi ya marketing
 
Hii ni internal vacancy announcement, wewe inakuhusu nini? Au hujui kizungu, hivi unafikiri ukikimbilia court unapata unachotaka tu, acha wivu wa fisi
Bado hujajibu hoja hakuna anayeona wivu zaidi haya mambo wasipo yazuia taasisi zote zitakuwa zinafanya hvyo tunaelekea wapi!!!...Jitafakari
1.kwann kipindi cha nyuma hawakutoa ajira !!walivyosikia neno kujitolea Bungeni wamezimwaga!!
2.Walikuwa wanalengo/maana gani kutoa kwa public wakati wanajua ajira ni za ndani kwa ndani hapa [emoji2955][emoji2955][emoji2955] kunamtu anatafutwa ...
Mwisho..
Waweke ushindani sote ni Watanzania
 
Mtoa hoja hakusema taasisi zisiajiri.
 
Manual manual ndo nn mzee! Hivi unajua hoja ya msingi hapa ni Nini!?? Hakuna aliyekataa hiyo manual yao ila iwe ya haki na usawa.. we nafasi 392 uwatafute tu uvunguni mwa nssf wakati kuna namba kubwa huko mtaani.... Alafu kun wajinga wanasema wenzenu wamejitolea nikuhakikishie tu hata hao waliojitolea humo nssf watakaopata hiz kazi ni 30% tu mtashangaa shele litakalochezwa hapa
 
Yaan hi ndo hasara yakuamka usingizin ukafungu Jf huku unawashawasha macho.. hapo ndo umeongea nn
 
Safi sana NSSF. Kwanini msijiajiri kwenye umachinga au bodaboda? Mnapenda kazi za ofisini tu siyo?. Mnataka hao watoto wa vigogo waendeshe bodaboda wapigwe vumbi kama ninyi au wapate ajali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…