Kutangaza nafasi za ajira kwa watu "Wa ndani ya NSSF" ni Ubaguzi, Rais Samia ingilia kati, unachonganishwa na wananchi!

Tatizo la watanzania ni kama mandondocha.
Hili jambo lilitarajiwa baada ya tume ya ajira kupokwa mamlàka ya kuajiri na taasisi kutaka zianze kuajiri direct.
Hapa ndipo mlitakiwa kupiga kelele!
Kwasasa ni kelele za chuma tu
Lazima watanzania kwa umoja wetu tukatae huu ubaguzi!! Haiwezekani kodi tulipe wote lakini kundi moja dogo lijifanye kana kwamba NSSF ni yao binafsi!! Wakiachwa wakafanikiwa katika ubaguzi huu Tanzania itakuwa ya mabaka!! Na taasisi zingine zitaiga huu ubaguzi wa NSSF, kijana akimaliza chuo tu anapewa kujitolea mahali au anapewa mkataba halafu baadaye anatangaziwa nafasi za ajira kwa "walioko ndani". Wengine wakimaliza chuo wanabanana mitaani wakati wenzao wameingizwa ndani!!
 
Ajira kupitia tume ya ajira ilipunguza sana urasimu pamoja na kuwa hakuna kitu kinakuwa sahihi asilimia mia.
Ni ngumu sana kwa taasisi kuajiri zenyewe direct kukakosekana undugunisation.
Ajira lazima zitaañzia kwa walioajiriwa kwanza.
Mfumo huu wa ajira ndio wakupigia kelele si vinginevyo, tena mapema kabla haujazoeleka.
Hata wakiwaita wote kwenye usaili bado watakaopata ajira ni walengwa tu.
 
Yaan hi ndo hasara yakuamka usingizin ukafungu Jf huku unawashawasha macho.. hapo ndo umeongea nn

Mbona wanaopeleka maombi wanapewa na ndiyo hao waliojitolea kwa muda zaidi ya mwaka sasa ulitaka upewe wewe roho mbaya tu na ulivyo kilaza wewe mtu wa kulialia utawezaje kuwa mtendaji bora, haya ni mashirika yanaendeshwa kwa taratibu hakuna mwenye mamlaka ya kuendesha shirika anavyotaka sio mali ya mtu wala sio ya baba yako ni mali ya umma,
 
Umeongea pointi tupu
 
1.samia ni dhaifu hawezi fanya chochote.

2.Ukizingatia pale wamejaa kobazi"Dauism".

3.Hakuna hatua yoyote itakayochukuliwa.

Mungu tumekukosea nini mpaka tunapewa rais dhaifu asiyejali raia wake?
 
Inaumiza sana, inauma sana Iv Sheria ni nini? Democracy ni nini? Tunu za taifa ni nini, kwanini haya mambo wanayapuuza Ivi, dharau za wazi wazi, watu wanalifanya taifa kama familia Yao! Lolote watakalo wanalifanya na hii iwekwe wazi ni dharau kwa Rais wetu, yote haya wanataka kumchafua Tu sio kwa huu uzembe wa NSSF.
 
Tuambie kidogo hiyo manual ya NSSF inasemaje kwenye kuajiri bila kushindanisha watu?

Bila kushindanisha watu?
Nop! Wanashindanishwa watu wa ndani kwanza.
Akikosekana mwenye sifa anatufutwa mtu wa nje.
That is how many employers retain and promote best employees.
Is this new to you?
Gosh!
 
unavyojua ww ubaguzi mpk wa rangi et....
Ila tabaka mwenye nacho na asikuwa nacho hamlioni et....
Hii nchi aliyesema mbinguni ni station ya vituko hajakosea....
Kwa hiyo Samia tunambagua kwa sababu ya tabaka. Samia ni tabaka gani, masikini ?

Mnashindwa kutueleza. Samia tunambagua kwa kipi, Samia ni albino ??????
 



NSSF - government private ATM (?)

Mahakama - government (conveniently) toothless dog (?)




Tuendelee ‘kumuomba’ Rais Samia.
 
sana kwa taasisi kuajiri zenyewe direct kukakosekana undugunisation.
Ajira lazima zitaañzia kwa walioajiriwa kwanza.
Mfumo huu wa ajira ndio wakupigia kelele
Eti leo ndio tumeamka.

Siku ile Rais alipotangaza mashirika yaajiri yenyewe hakuna aliyehoji.

Maamuzi makubwa makubwa ya kitaifa anaachiwa yule Mama. Watu Milioni 60 tunaweka rehani maisha yetu kwenye kichwa cha mtu mmoja.

Dhana na zama za "Zidumu Fikra za Mwenyekiti wa Chama" bado tunazo.
 

Us common wananchi still believe in huruma ya Rais.

Bado tunaogopa hata Mahakama tukidhani ni nyumba ya wahalifu na majambazi tu.


Elimu ya kujitambua na kutambua haki na wajibu ilifutwa ama haikuwahi kuwepo?

Kila mtu analia hakuna aliye tayari kutuonyesha kwa vitendo haswa.
 
Shida hakuna namna nzuri ya kupata hizo ajira za kujitolea
Watu wanatumia gap hilo kuingiza ndugu zao
 
Hizo ni dharau sasa.
Hayo maamuzi ulitaka uachiwe wewe
Kumbe ni mjinga sana wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…