Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Mimi bado nashangaa Kama wengine wanavyoshangaa.....kuwa ukiwa na picha ya Rais unashinda mechi yako.au kutoa draw. Nashauri Yanga waende nazo Tunisia
Mashabiki wa Timu zote wanamkubali mh Rais wetu mpendwa mama Samia maana Ni mwana michezo pia ndio maana unaona amekuwa akifuatilia kwa karibu Sana pale timu zetu zinapocheza iwe ndani ya nchi au nje ya nchi
 
Kwa katiba hii tuliyonayo, kila kiongozi atakayepata fursa ya kuwa Rais na kuiongoza taasisi nyeti ya urais, basi ni lazima watatokea tu wapambe wa kumsifu na kumuabudu, japo huo ni wajibu wake kikatiba pale atimizapo majukumu yake ya kila siku.

Hii ilikuwa ni hivyo hata wakati wa BWM, JK, JPM na hata sasa wakati wa SSH. Japokuwa haikuwa kitu cha kawaida sana wakati wa tawala za JKN na AHM.

Hata akija Mwigulu au Makamba baada ya SSH, watatokea tu wapambe na kuendelea kutoa sifa kama hizo. Hata awe Kibajaji ama Msukuma hawatakosena chawa wao.
 
Kama kiongozi anafanya vizuri na kutekeleza majukumu yake vizuriii ni lazima apongezwe kwa kuwa siyo wote wenye kutimiza wajibu wao wapewapo, hivyo anapotokea kiongozi aina ya Rais mama Samia aliyejitoa na kujitolea kuwatumikia watanzania wanyonge kwa nguvu zake zote na muda wake wote lazima tumpongeze na kumuunga mkono juhudi zake za kutukwamua kiuchumi watanzania, Haipaswi kumkatisha Tamaa bila sababu, haipaswi kumvunja moyo, Haipaswi kumkwamisha kwa makusudi maana kumkwamisha Rais Samia Ni sawa na kuwakwamisha watanzania wote
 
Kwani kuongea ukweli ndio uchawa? Kwa hiyo wewe hapo unapinga pinga kila kitu ili upate faida gani? Tusijenge Tabia ya kuwakatisha Tamaa viongozi aina ya Rais Samia waliojitoa na kujitolea kututumikia watanzania kwa uzalendo mkubwa
Uteuzi
 
Duuh!! Unashindwa kusifu, kuabudu, kumuimbia na kumchezea Mungu wako,badala yake unamgeuza binadamu mwenzako "mungu"!!!???

Kweli umasikini wa akili na kipato ni vitu vya kutorithisha watoto wetu.

nakuunga mkono sana, umasikini ni kitu kibaya sana na ndio chanzo pia cha maujinga mengi kwenye nchi hii... Wenye mamlaka wanapambana kuhakikisha watu wanadhidi kuwa masikini kifikra na kiuchumi ili wawatawale vizuri.

Tupige vita umasikini wa fikra na kiuchumi kwa vizazi vyetu.
 
Kijana acha tabia za kunyenyekea watu na kuabudu watu baadala yake ishi na simamia kweli na thabiti, huu ushabiki ushabiki dhidi ya wanasiasa ambao wameamua kuifanga nchi sehemu ya mali za familia na koo zao ni mbaya sana na tuuache mara moja.

Tabia hizi za hovyo hurithiwa na familia yako matokeo yake unakuwa na watoto wajinga watakaokuja kuishi kama wapambe aka chawa wa watu huku wenzao wakichuma na familia kwa kuendelea kunyonya mamilioni ya watu.
 
Chema chajiuza, kibaya chajitembeza, kwa mbali nakumbuka picha za Mwigulu kwenye nguzo za umeme, kwenye mitaro, kwenye barabara na madaraja hadi kwenye miamba mlimani.
 
Hata ije tume kutoka marekani kusimamia uchaguzi bado Rais Samia atashinda kwa kishindo maana anakubalika na kupendwa Sana na watanzania

Huko Marekani mbali, hii hii lakini ifanye kama tume huru ya uchaguzi ya Kenya, hapo ndio utajua CCM ni chama outdated.
 
Mleta mada ulipokuwa mtoto naamini ulikuwa na ndoto nyingi, kubwa na ndogo. Pengine wazazi nao walikuwa na matamanio yao kwako.
Usikate tamaa, hujachelewa bado.
 
Back
Top Bottom