Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Kutawala kwa picha ya Rais Samia uwanjani ni ishara ya mafanikio katika kujenga umoja wa kitaifa na kukubalika kwake

Ndugu zangu Rais Samia hakika amefanikiwa kujenga umoja wa kitaifa, amefanikiwa kuliunganisha Taifa, amefanikiwa kuwaweka watanzania pamoja, amefanikiwa kuishi katika mioyo ya watanzania , Amefanikiwa kupanda mbegu ya Uzalendo katika mioyo ya watanzania

Sasa picha ya Rais Samia inashangiliwa uwanjani Tena katika mchezo mkubwa siyo tu Tanzania Bali katika Bara Zima la Afrika, picha ya Rais Samia inaleta furaha na Tabasamu kwa mashabiki uwanjani, picha ya Rais Samia inakuwa sehemu ya burudani na furaha ya mchezo, mashabiki wote wa timu zote wanafurahi kuona picha ya Rais Samia ikiwa inapepea uwanjani

Hii ni kutokana na kuwa kila mtu na kila shabiki wa mpira anamuona Rais Samia kuwa Ni Rais wake na kiongozi wake, Hakuna mwenye chuki na Rais Samia, Hakuna mwenye kinyongo na mama Samia, hakuna mwenye Hasira na mama Samia. Kila Shabiki akiona picha ya Rais Samia mbele ya uwanja anaona furaha na Tumaini, kila mtu anahisi Rais Samia Ni mshabiki wa timu yake na anajisikia fahari,

Hakika Rais Samia Ni kipenzi Cha watanzania, Ni Tumaini la watanzania, furaha ya watanzania ,kiongozi aliyeteka mioyo ya watanzania, kiongozi anayekubalika na watu wote vijana kwa wazee. Ukifanikiwa kupenya katika mioyo ya wanamichezo maana yake umefanikiwa kukaa katika mioyo ya watanzania maana mchezo wa mpira ndio mchezo unaopendwa na watu wengi Sana Tanzania na unao waunganisha watu bila kujari itikadi zao za kisiasa

Kazi iendeleee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na sauti

Lucas Mwashambwa, kijana mzalendo na mpenda nchi yangu
Mazuri hayaigwi ila yenye ukakasi yanastawi uhuru wa kisiasa sifuri, mishahara sifuri, Bata wale wao, kejeli zao, makanisa yasijengwe, umeme shida, mfumuko wa bei, vifo vyaajali za barabarani, Hivi ndivyo kulivyo nchini Guetemalata na Bamsenene.
 
ni tabia za kike ndio zinawasumbua mashabiki wetu! duniani kote mpira unapigwa lakini huwezi kuona picha za marais wao! pale mchezo wa soka ambao rais wake ni karia ,motsepe,na infantinho,kwa nn wasibebe mabango ya hao? shame!
Ishara ya unpopular na fursa za machawa, ukionekana unafagilia hata huku Guatemalata hali iko hivyo, madume na majike wamekataa mazima.
 
Mazuri hayaigwi ila yenye ukakasi yanastawi uhuru wa kisiasa sifuri, mishahara sifuri, Bata wale wao, kejeli zao, makanisa yasijengwe, umeme shida, mfumuko wa bei, vifo vyaajali za barabarani, Hivi ndivyo kulivyo nchini Guetemalata na Bamsenene.
Kwani Nani amekuzuia kujenga Hilo kanisa unalolilia kulijenga, fuata utaratibu Jenga kanisa lako, suala la mfumuko wa Bei limeshughulikiwa vizuri kabisa na mh Rais wetu mpendwa, mfano katika kilimo tunaona namna mh Rais alivyotoa mabillioni ya pesa Kama Ruzuku na kupelekea mbolea kushuka Bei sokoni zaidi ya nusu ya Bei ya mwaka jana
 
Mwagito, Niko Guatemalata hayo huku sijayaona endelea kuboresha huko kwenu, bei ya mchele, viazi, unga, mahindi, sukari? Vipi huko sisi huku tumepewa neema ya vilevi ndio havina mfumuko wa bei, ibada ya kumwagilia moyo imeenziwa vizuri, tunashukuru hapa Guate city tuko sawa.
 
Ndio nchi nyingine wenyewe wametuzidi sisi maana wenyewe Wana Tabia na utamaduni wa kumpongeza kiongozi pale anapofanya vizuri na hata Kama Ni kukosoa wanaweza wakakosoa utekelezaji wa Sera lakini wakaunga mkono Sera husika,

lakini huku kwetu unakuta mtu kazi yake kuanzia January Hadi December nikupingaa tu kila kitu na kila Jambo, kila Sera na kila ajenda ni kupinga tuuu bila sababu Wala hoja za msingi, ndio sababu unaona hata wananchi kwa Sasa wanawapuuza wapinzani na upinzani
Hapo uko sahihi.
 
Hoja yenye ukweli haiwezi kumgeuza mleta hoja kuwa mjinga, kinachohitaji kwako Ni kubadilika kifikira na kimtizamo na mawazo potofu uliyo nayo kichwani ili uanze kuona kwa akili yako halisia na Timamu mambo makubwa aliyoyafanya mh Rais wetu

Hoja ndo hiyo? Au hoja ni picha na Ile aliyoongea mleta Mada?
 
Back
Top Bottom