Kutoa kwenye ATM kwango cha laki nne kwa mkupuo mmoja ni kidogo sana, nashauri waongeze

Kutoa kwenye ATM kwango cha laki nne kwa mkupuo mmoja ni kidogo sana, nashauri waongeze

Ndiyo uhuni huo tunaozungumzia ,hadi noti zinaisha hawaoni?

Nakuelewa, kumbuka hakuna mtu anakaa kuhakikisha Pesa zipo kiasi Gani kwenye ATM na matumizi yanatofautiana kulingana na nyakati. Mfano, mwisho wa mwezi na mwanzo wa mwezi matumizi ya ATM Yana tofautiana. Hapo hatujaongelea weekends napo watu wanaotumia sana Kwa vile bank zinafungwa mapema au Kuna siku hazifunguliwi. Hauwezi kuepuka Mara Moja Moja kukuta ATM Haina pesa au inawekewa pesa wakati wewe unasubiria huduma.
 
Benki kupitia mashine zao za ATM wamekuwa na ukomo wa kiwango cha kutoa pesa. Kutoa kwa mara moja kiwango cha juu ni Laki nne.

Yaani kutoa Milioni moja mpaka uweke kadi mara 3 huu ni upotevu wa muda na ongezeko la gharama kwa wateja.

Kwa niaba ya wateja wenzangu ninaomba kiwango kiongezwe.
kuna baadhi ya atm za crdb zinatoa laki 6 kwa mkupuo
 
Kuna wakuu hapa either wanakurupuka au hawajui nini wanajibu.

Mtu anasema inawezekana ila hasemi Bank na mfano wa ATM mbona, wadau wamejaribu bank nyingi tu na bado limit ni hiyo laki 4.

Kama unamfano wa ATM na Bank weka hapa watu wakajaribu kutoa hizo Million kwa mkupuo.
 
Wapi huko?
Obama Avenue pale nyumba ya HQ... mambo iko hivi

WhatsApp Image 2024-09-30 at 18.49.28.jpeg
 
Benki kupitia mashine zao za ATM wamekuwa na ukomo wa kiwango cha kutoa pesa. Kutoa kwa mara moja kiwango cha juu ni Laki nne.

Yaani kutoa Milioni moja mpaka uweke kadi mara 3 huu ni upotevu wa muda na ongezeko la gharama kwa wateja.

Kwa niaba ya wateja wenzangu ninaomba kiwango kiongezwe.
CRDB ni 600k,huo ujinga uko NMB
 
Benki kupitia mashine zao za ATM wamekuwa na ukomo wa kiwango cha kutoa pesa. Kutoa kwa mara moja kiwango cha juu ni Laki nne.

Yaani kutoa Milioni moja mpaka uweke kadi mara 3 huu ni upotevu wa muda na ongezeko la gharama kwa wateja.

Kwa niaba ya wateja wenzangu ninaomba kiwango kiongezwe.
NMB ni laki 2
 
Limitation Iko kwenye technology, most ATM machine can dispense upto 40 bills (noti) ndio sababu ya msingi. Japo sokoni kuna new model Zina toa mpka note 100 siyo nyingi, tunaelekea huko.

Upande mwingine kutoa kiduchu kiduchu kibiashara Ina make Sense bank wanapata miamala mingi.
 
Ila benki zetu zina mambo ya kifala sana asee juzi nimekwazika nikaamua kutoa hela zangu zote na sasa ni bora tu maana nimetengeneza kibubu cha chuma hicho sitakatwa hata mia yangu, Haiwezekani watu wananiita nikahakiki taarifa za acc yangu then navunja ratiba zangu nafika pale napangishwa foleni kama mkimbizi masaa matatu alafu mara mlinzi anigasigasi mara toa kofia,mara usisimame hapa kasimame pale, mara mwingine ahudumu kama hataki yaani nikachoka maana hawa wahudumu wote wanalipwa hela ninazokatwa mimi alafu wananitreat kama mdoli wao tu… nikaangalia ile picha ya majority ya walio kwenye foleni nikagundua tupo kama manyumbu asee haya masuala ya benki labda nije kuwa bilionea ila ukiwa milionea kushuka chini bado tabu tupu bora kuhifadhi hela zangu kwenye kibubu, Sitapanga mafoleni ya kiwaki kupata hela yangu tena, Wala sitakuwa na haja ya kusafiri kutafuta sehemu ya kutoa hela zangu tena, Pia nitakuwa nina uhakika na usalama wa hela zangu maana kwa sasa sioni ajabu mtu anaweza kudukua tu akachomoa hela zote ukaja kushtukia simbank inakutaarifu kuwa umetoa kiasi fulani na hujafanya hivyo, Kwa sasa kero za makato ya kila mara hadi ninapotaka kuangalia akiba yangu sitakuwa nayo tena kmmake.

Wenye hela hata hawakai foleni, Nimeshuhudia wanapewa huduma kwa njia ya simu tu wakiwa maeneo yao nyumbani wala hawana haja ya kwenda bank alafu wanaweza tu kutuma mtu

Ukiona benki hupati special treatment ujue wewe ni mjinga na unanyonywa tu hela zako
 
Back
Top Bottom