Ila benki zetu zina mambo ya kifala sana asee juzi nimekwazika nikaamua kutoa hela zangu zote na sasa ni bora tu maana nimetengeneza kibubu cha chuma hicho sitakatwa hata mia yangu, Haiwezekani watu wananiita nikahakiki taarifa za acc yangu then navunja ratiba zangu nafika pale napangishwa foleni kama mkimbizi masaa matatu alafu mara mlinzi anigasigasi mara toa kofia,mara usisimame hapa kasimame pale, mara mwingine ahudumu kama hataki yaani nikachoka maana hawa wahudumu wote wanalipwa hela ninazokatwa mimi alafu wananitreat kama mdoli wao tu… nikaangalia ile picha ya majority ya walio kwenye foleni nikagundua tupo kama manyumbu asee haya masuala ya benki labda nije kuwa bilionea ila ukiwa milionea kushuka chini bado tabu tupu bora kuhifadhi hela zangu kwenye kibubu, Sitapanga mafoleni ya kiwaki kupata hela yangu tena, Wala sitakuwa na haja ya kusafiri kutafuta sehemu ya kutoa hela zangu tena, Pia nitakuwa nina uhakika na usalama wa hela zangu maana kwa sasa sioni ajabu mtu anaweza kudukua tu akachomoa hela zote ukaja kushtukia simbank inakutaarifu kuwa umetoa kiasi fulani na hujafanya hivyo, Kwa sasa kero za makato ya kila mara hadi ninapotaka kuangalia akiba yangu sitakuwa nayo tena kmmake.
Wenye hela hata hawakai foleni, Nimeshuhudia wanapewa huduma kwa njia ya simu tu wakiwa maeneo yao nyumbani wala hawana haja ya kwenda bank alafu wanaweza tu kutuma mtu
Ukiona benki hupati special treatment ujue wewe ni mjinga na unanyonywa tu hela zako