Kutoa kwenye ATM kwango cha laki nne kwa mkupuo mmoja ni kidogo sana, nashauri waongeze

kwani hii ina effect gan mkuu
Tanzanite ndio ya kawaida limitation kibao mfano kiwango cha kutoa hela, limitation za online purchases na “normal” customer service

Titanium unyama unaanzia hapa.

World aka Black unyama unafika kikono hapa.


Kujibu swali lako narudi sasa hivi mkuu.
 
Kile kishimo cha kupitisha hela, mwisho wake ni bando lenye unene gani?
 

Mkuu ushawahi kufanya kazi BANK? Unajua kwamba kuna monitoring ya hizo fedha? Wewe unafikiri mpaka mtu achungulie ndiyo ajue kwamba noti zimeisha za elfu 10 au 5? Katika ulimwengu huu wa gidital mpaka uende kwenye ATM uchungulie ndiyo ujue hela hakuna? Wanaoweka fedha kwenye ATM wanajua matumizi ya hizo ATM katika vipindi vyote maana wana trends za uchukuaji hela wa wateja ,kwahiyo ukiona hadi fedha hakuna kwenye ATM jua wazi kwamba kuna uzembe wa 100% umefanyika.
 
Kama wao wahuni hifadhi pesa zako chini ya godoro kwako
Mkuu nina muda mrefu sana sijwahi kutoa fedha kwenye ATM ,mimi natumia sana miamala ya simu ,account yangu sijui hata kama inafanya kazi maana muda mrefu sana sijaitumia.
 
Hizi benki zetu zinapenda makato ndiyo maana hawataki uchomoe kwa mkupuo wakukate ya kutolea alafu mwisho wa mwaka wanatangaza faida.
 
Sizungumzii hao wa 15,000 au 25,000 hata ukitaka kutoa laki 400 kwa pamoja hauwezi kwasababu wameweka elfu 5 tupu hivyo itakulazimu utoe laki 2 tu.
kwahiyo hapo juu unamaanisha ATM haziwekwi noti za elfu 10.! nadhani haupo sahihi kwanza ni ATM ya benki hani hiyo unayosemea wanaweka noti tupu za elfu 5000 kila siku
 
kwahiyo hapo juu unamaanisha ATM haziwekwi noti za elfu 10.! nadhani haupo sahihi kwanza ni ATM ya benki hani hiyo unayosemea wanaweka noti tupu za elfu 5000 kila siku
Huwa wanafanya uhuni wa kuweka elfu 5 ili wapate fedha nyingi kwenye ATM charges.
 
Kwanza tujiulize lengo la ATM kuanzishwa. Hazikuja kuwa mbadala wa kutoa hela benki kwa teller, zimekuja kuondoa usumbufu wa mihamala midogo hiyo ya laki laki ngapi.

Vilevile ATM haiwezi wekwa noti nyingi sana kutosheleza nyinyi mnaotaka kutoa milioni mbili mbili, mkija watu 20 kwa siku wa kutoa milioni 2 si magari ya fedha yatashinda yanasomba hela kupeleka ATM za mitaani?

ATM zipo kwa miamala midogo, zihudumie watu wengi ila wanaotaka hela nyingi waende matawi ya benki. Mnalaumu tu bila kutazama uhalisia.
 
Lengo lao ni makato ukitaka kutoa 1M itabidi utoe mara 3 na zote kuna hela wanakata
 
Sisi wa tigopesa hii haituhusu....unatoa mil 5 shwaa
 
Pesa ingekua inatoka in-term of Dollar!! Halafu watu wa Exchange wawe kila mahali kama Maagent...

Unatoa nyingi kwa mara 1
 

Ule mdomo wa ATM hasa za zaman ulitengenezwa kutoa maximum ya Noti 40 ndo mana kama ni Noti ya elfu kumi basi utatoa Noti 40 yaan 400,000 na kama ni Noti za elfu 5 basi utatoa laki mbili tu.hizi ATM mpya ndo naona zimeanza kutoa pesa nyingi Kuna ATM apa apa Bongo inatoa mpaka million Moja kwa mara moja.sema wali disable isitoe zote kwa mara Moja ili mabank yavune charges.mana ukitoa laki nne unakata kama 2,000 ivi au below.Ndo ivi mabank watakula wapi ni lazima wawe wabunifu
 
laki 4 kwa watu 50 kwa kutwa ni mil 20.

Atm inapaswa kuwa na Sh ngapi kwa watalaam?

Kwa mujibu wa Mtandao, ATM za kizamani kabisa zilikuwa zinapokea 20mil, ila ATM za kisasa zaweza kupoka hela nyingi. Ni uwezo tu wa bank kuzitosheleza....
 
Hivi nikitaka niwekewe ATM nyumbani kwangu utaratibu ukoje manake wengine matumizi yetu hadi sheitwani anatuogopa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…